JIMBO LA NGARA CCM-2015:-Alex Rafael Gashaza ashinda kwa kura nyingi dhidi ya Issa Husein Samma na Mama Helena.
Wafuasi wa Mgombea Udiwani kata ya Rusumo ,wilayani Ngara mkoani Kagera,Bw.Wilbard Mbambara wakiwa na shamrashamra baada ya kuibuka Mshindi katika kura za maoni zilizofanyika jana Agosti 01,2015.
Jana Agosti 01,2015 ilikuwa ni kufa au kupona kwa makada wa CCM wanaowania ubunge wakati wanachama wa chama hicho tawala nchini Tanzania walipopiga kura wilayani kuchagua wagombea kwenye majimbo yao baada ya siku 10 za vikumbo zilizojumuisha kurushiana ngumi, tuhuma za rushwa na malumbano wakati wa wagombea hao kujinadi kwa makada wenzao katika kata mbalimbali za majimbo wanayotaka kugombea.
Akizungumza na Mwanawamakonda Blog,Katibu Mkuu wa CCM wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Jacob Makune,amesema uchaguzi huo umeenda vyema ambapo wameisha pokea matokeo ya vituo vyote 112 kutoka Matawi 107 na waliotarajiwa kupiga kura ni 50,717,waliopiga kura 32,589,kura zilizoharibika 566 na kura halali ni 32,023.
MATOKEO KURA ZA MAONI JIMBO LA NGARA CCM-2015.Â
1.     Bw.Alex Rafael Gashaza -  kura 10,814.
2.     Bw.Issa Hussein Samma kura – 7,166.
3.     Bi.Hellena Adrian Ghozi – kura 5,474.
4.     Dr.Philmoni Sengati â kura 4,363
5.     Mwl. Jerad Muhile â Kura 1866
6.     Bw.Cyprian Muheranyi â kura 927
7.     Bw.Ladislaus Bambanza â kura 636
8.     Bw.Wilbard Eden Ntamahungiro â kura 390
9.     Bw.Joachim Nchunda â kura 357.
Bw.Makune amesema baada ya  Mchakato wa kura za maoni, utafuatiwa na vikao vya kamati za siasa za wilaya na mikoa wakati kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kitafanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 11 kwa ajili ya uteuzi wa wagombea rasmi wa ubunge na udiwani wa CCM.
Uchaguzi Mkuu Tanzania umepangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,2015.
Recent Comments