Recent Comments

CHANGAMOTO YA MAJI RULENGE NGARA

By Simamia Ngara Jul 12, 2024

HABARI PICHA

Pichani ni Mwananchi wa eneo la Kagazi katika mamlaka ya Mji mdogo wa Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera akichota maji kwa kutumia kikombe na chujio kwaajili ya kuchuja uchafu uliomo katika maji hayo.

Aidha changamoto ya maji bado inawakabali wakazi wa wilaya ya Ngara katika maeneo mengine ambapo wanachi kulazimika kutumia maji ambayo siyo safi na salama Kwa afya zao huku maji yaliyo safi na salama yakipatikana umbali mrefu.

Hivyo basi sera ya kumtua mama ndoo kichwani bado inahitajika kufika mahali ambapo bado kuna uhitaji wa huduma mhimu ya maji.