Recent Comments

#CORONAVIRUS-MAREKANI: WAGONJWA WAPYA ZAIDI YA 22,900 WAMERIPOTIWA JANA

By ObyMack David Jun 12, 2020

Marekani imeripoti wagonjwa wapya 22,921 kwa siku ya jana Juni 11, 2020 idadi inayofanya jumla ya maambukizi kwa Taifa hilo kufikia 2,654,827

Idadi hiyo inajumuisha idadi ya visa kutoka Majimbo yote 50, District of Columbia, maeneo mengine yaliyo chini ya marekani na wagonjwa Wamarekani walitoka mataifa mengine

Taifa hilo la Amerika ya Kaskazini kwa siku ya jana pia limetangaza jumla ya vifo 894 na kufanya kuwepo kwa jumla ya vifo 119,349 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Hata hivyo, Marekani inayoongoza Duniani kwa idadi ya vifo na maambukizi imeripoti jumla ya Wagonjwa 777,350 walipona #COVID19 hadi kufikia leo

#COVID19USA #USA #Updates