ADAM MKWEPU NA VERONICA ROMWALD
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa amesema hana haja ya kuwazungumzia viongozi wanaomaliza muda wao madarakani, badala yake anamlenga kiongozi atakayekuwa rais wa nchi kwa miaka mitano ijayo.
Dk. Slaa alisema hayo Dar es Salaam jana katika mahojiano maalum na mwandishi mkongwe, Tido Mhando wa televisheni ya Azam.
Akijibu swali kuhusu kwa nini anamzungumzia tu mgombea urais wa Chadema anayewakilisha Ukawa, Edward Lowassa badala ya kuzungumzia ufisadi kama mfumo mzima wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Slaa alisema:
âTido, nilielezea juu ya Serikali ya CCM akiwamo Rais Kikwete (Jakaya) ndiyo iliyomlea Lowassa (Edward)⦠John Mnyika bungeni aliwahi kusema Kikwete ni dhaifu hilo halina utata, lakini hivi sasa hatumzungumzii Kikwete kwa kuwa anaondoka na ameshaagwa.
âTunapoteza muda kwa mtu ambaye kesho hayupo, hapa tunamzungumzia mtu ambaye tutakuwa naye kama rais wetu kwa miaka mitano ijayo,âalisema Dk. Slaa.
Kuhusu kuwataja mafisadi wengine, katibu mkuu huyo wa zamani wa Chadema alisema hajawahi kupata kigugumizi cha kuwataja mafisadi na kudai kwamba aliwahi kuwataja baadhi ya viongozi kwa ufisadi ndani ya ofisi ya Ikulu kwenye mikutano ya hadhara na hakukamatwa kwa kuwa alifanya utafiti.
âNazungumzia hawa kwa kuwa madhara (impact) yao ni kubwa kuliko hao wengine lakini tutaendelea kuwapigia kelele kama ilivyo kwa watumishi wengine hadi wakaondolewa kwa hiyo tulikwenda kuwataja watu na sikumungâunya maneno,âalisema.
Katika mahojiano hayo maalum, Dk. Slaa alikiri kwamba alihama nyumbani kwake kwa muda kutokana na vitisho dhidi yake na kudai kuwa alitoa taarifa ya kupatiwa ulinzi kuhakikisha usalama wake.
âNi kweli na ndiyo maana sikuficha kama nilikuwa Serena hata hivyo sikuona kuwa ni kitu cha ajabu na mbona watu hawajiulizi kwamba 2010 kipindi nagombea urais nililala Serena kwa nini leo liwe jambo la ajabu wakati hii si mara yangu ya kwanza,âalisema Dk. Slaa.
Recent Comments