Naomba kuwashukuru woote ambao mmenipongeza na kuahidi kuniunga mkono katika nia yangu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Ngara.
Tangu nimesema rasmi juu ya Nia yangu hiyo, nimepokea simu na messages nyingi za kuniunga mkono, zaidi ya ambavyo nilitarajia.
Hata hivyo, kwa masikitiko makubwa sana, naomba kutoa taarifa kuwa, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, nimeamua kuondoa jina langu katika kinyang’anyiro.
Kwa hatua hii, ninawatakia kila la heri Watia Nia wote, na niko tayari kushirikiana na yeyote mwenye lengo jema kwa ajili ya wilaya yetu ya Ngara.
Nitaendelea kuwatumikia Wana-Ngara kupitia taaluma yangu ya habari, na kupitia nafasi yangu niliyonayo katika Chombo Kikubwa cha Habari hapa Nchini ambacho ninakifanyia kazi.
Ninawaomba radhi saaaana wote ambao kwa namna moja ama nyingine watakuwa ‘disappointed’ na huu uamuzi wangu.
Recent Comments