Aliyewahi kuwa rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) Fatma Karume ambaye pia ni mwana harakati amekipongeza chama cha mapinduzi (CCM) kwa kufugua kituo chao cha mawasiliano kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mapema mwezi Oktoba mwaka huu.
Karume ametuma pongezi hizo kupitia ujumbe wake aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kuhoji iwapo chama hicho hakitatuma polisi kama vyama vingine vya upinznai vikiamua kutengeneza vituo vyao vya mawasiliano kama walivyofanya kwenye uchagzi uliopita.
âVery good. CDM na ACT na vyama vengine wakiwa na VITUO VYA MAWASILIANO hamtotumia POLISI kuwavamia kama mwaka 2015? Maana mkuki kwa nguruwe kwa Binadamu mchunguâ ameandika Karume.
Chama cha mpinduzi kimezindua leo kituo chao cha mawsilisano kwa ajili ya kutuma taarifa za uchaguzi kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa kampeni za uchaguzi mkuu baadaye mwezi huu.
Recent Comments