Recent Comments

FOLENI YA MADUMU YANAYOSUBIRI KUJAZWA MAFUTA YAGEUKA KERO NGARA

By Mwafrika Aug 5, 2024

Simamia.com imetenbelea moja ya kituo cha kuhudumia mafuta na kujionea Hali isiyo ya kawaida,Hali hiyo ni kukithiri Kwa foleni ya Watu wenye Madumu mengi ambayo sio sahihi Kwa Usalama.

Camera Nene iliongea na moja ya Mkazi wa kabanga aliyeenda kuchukua mafuta kwenye pikipiki lakini amekosa huduma hiyo baada ya Foleni ya Madumu kukithiri na mengi yanasadika yamaenda kuuzwa Burundi.

Picha ikionesha Madumu yaliyopo kwenye foleni ya mafuta

Mwananchi mwingine ambae jina lake Tumelihifadhi baada ya KUOMBA kutotajwa amesema”Hawa majirani zetu wa nchi jirani hatuwazuii kuja kufuata mafuta ila tatizo wanakuja na Madumu na kufanya biashara jambo Ambalo linatukera na kufanya tunakosa huduma na kazi haziendi”.

Uchunguzi wa Simamia.com unaonesha kua Kumekua na kasumba ya Wafanyabiashara wasio na vibali Wala hawalipi Kodi ya Serikali lakini wanafanya Biashara ya mafuta kinyume na taratibu na bei elekezi.

Kuna gari moja la Burundi limechorwa picha za Chupa za Vileo(Pombe)lakini linabeba mapipa ambayo likifiks kabanga linajazwa mafuta na kupeleka Burundi kufanya biashara.

Simamia Media na simamia.com inaishauri Serikali na viongozi wa mpakani kabanga kuchukua hatua a haraka kwani maisha ya wananchi na wakazi yanapanda Kwa kukosa huduma hiyo ambayo inaonesha Kuna wanaonufaika huku wakifanya biashara kinyume na taratibu na Sheria za Tanzania.

Muda huu baada ya Walinzi wa moja ya kituo cha kujazia mafuta kuona watu wakawashtua waliokuja na Madumu na kuyaficha lakini simamia.com na Camera Nene imeshafanikiwa kupata picha na video fupi ambazo zimetunzwa kama ushahidi wa tukio Hilo Ambalo limetokea Leo tarehe 5/8/2024.