Ngara ni wilaya ambayo bado imebarikiwa mvua ambapo mvua zilizo tarajiwa kunyesha kati ya mwezi Agost na Septemba hatimae zaanza kunesha katika kata ya Kabanga, simamia.com imeshuhudia alfajiri ya tarehe 4-9-2023 mvua zikinyesha katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Hata hivyo hii ni neema kwa wakulima wamazao mbalimbali wa mazao mafupi ambao walikua wamesha lima kwaajili ya kupanda mahindi na maharage kuanza kupanda na kwa wakulima wa mazao ya muda mrefu kama vila Parachichi,Ndizi na mii ya kibiashara wakifurahia mvua hiyo.
Vilevile mvua hiyo imesaidia kupunguza vumbi ikizingatiwa kuwa wilaya ya ngara barabara zake nyingi ni za vumbi ambapo mvua hizo zilikatika kati ya mwezi Aprili na mwezi mei hivyo watumiaji wa barabara hizo wamekua wakikutana na vumbi kwa kipindi chote hicho.
Pia Ngara ni wilaya ambayo wakulima hupata kulima misimu miwili ya mvua ambapo msimu wa kwanza kuanza mwezi Septemba mapaka mwezi Januari na msimu wapili huanza mwezi Februari mpaka mwezi mei.
Lakini pia ujio wa mvua hizi kutapunguza changamoto ya maji ambapo wakazi wengi wa wilaya ya Ngara hasa kata ya Kabanga wanasumbuliwa na changamoto ya maji hivyo mvua hii itaenda kuwasaidia watu kupata maji.kumbukwe kuwa wialya ya Ngara ni wiaya ambayo bado inategemea kilimo cha mvua kwa kiasi kikubwa hivyo ujio wa mvuaa hizi ni neema na Baraka kwa wakulima wote wa wilaya ya Ngara na kilikua kilio cha wakulima wa wilaya hii.
Recent Comments