WILAYA ya Ubungo inatajwa kuwa ya pili kwa wingi wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliojitokeza kuwania nafasi za ubunge katika majimbo ya Kibamba na Ubungo, ikiongozwa na Iringa.
Hadi leo saa kumi alasiri wilayani humo, takribani wanachama, walishachukua fomu hizo ambapo 137, kati yao ni jimbo la Kibamba huku wengine 88, walichukua kwa ajili ya jimbo la Ubungo.
Kinyang’anyiro hicho kinatajwa kuwa na mchakato mkali kufuatia namba ya wanachama hao, huku baadhi ya wagombea wakihofia kuzungumza lolote kwa kile wanachosema kuwa ni haramu kwa miiko ya chama hicho kunadi sera kabla ya mchakato wa ndani wa chama kukamilika.
Wingi wa wanachama hao pia unaelezwa kuwa ahueni kwa wanachama hao waliochukua fomu kwani kuongezeka kwa wanachama wanaochukua fomu hakuongezi idadi ya wapiga kura hivyo kutakuwa na mgawanyo wa kura.
Roberts Muganzi, aliyechukua na kurejesha fomu ya kuwania jimbo la Kibamba, alisema idadi kubwa ya wagombea haiongezi isadi ya wapiga kura, hivyo kura zitagawanyika na kusababisha urahisi wa kushinda kwa wenye nia ya kushindana.
Alisema anadhania sababu ya kuongezeka kwa wanachama hao katika kinyang’anyiro hicho cha mwaka huu, kumetokana na kuwepo kwa ombwe la uongozi katika majimbo ya wilaya hiyo hivyo kumfanya kila mwanachama ajione anatosha zaidi ya waliokuwepo awali.
“Imedhihirika kuwa mwamko wa wanaochukua fomu zaidi ni kwa vijana hii pia nadhani inatokana na kuona vijana wenzao waliobahatika kuteuliwa na Rais wanavyochapa kazi hivyo wanawania ili nao waonyeshe uwezo wao na wakipata nafasi huenda tukashuhudia makubwa zaidi,” alisema.
Naye mmoja wa wagombea ambaye ni mlemavu wa macho Elia Msoke, alisema Demokrasia inaendelea kudhihirika ndani ya chama hicho, wingi wa wanachama wanaojitokeza kugombea ndio ishara ya demokrasia iliyotukuka kwa CCM.
Alisema yeyote anayehofia kushindwa kutokana na wingi wa waliochukua fomu huyo so muumini wa Demokrasia wakati ndani ya chama hicho imetawala.
Aliongeza kuwa wenye ulemavu wameona fursa ya kuwania nafasi hiuo kutokana na usawa katika chama hicho.
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Chief Yaredi, alisema watu wanaendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo, huku wao wakijipanga vyema kutenda haki katika kinyang’anyiro cha uteuzi.
Alisema tayari wameshapokea wanachama 225 kutoka majimbo yote, ambapo 137 kutoka Kibamba na 88 kutoka Ubungo.
Aliongeza kwa kuwataka wanachama kuendelea kujitokeza kwani bado wanazo fomu na muda wa kutosha kwa ajili yao, na kwamba wapo ambao tayari wamesharudisha fomu hizo.
Recent Comments