Mamlaka ya Kenya imetuma jeshi kusaidia zima moto katika kupambana na moto mkubwa ulioibuka katika hifadhi kubwa ya wanyama pori ya Tsavo ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii nchini humo.
Mamlaka ya huduma za hifadhi za wanyama pori imekilaumu kikosi cha zima moto kwa kushindwa kuzima moto huo ambao umekuwa ukiendelea kwa siku kadhaa.
Kwa sasa wanajeshi wanatumia helkopta kumwaga maji kuzima moto huo, wakati mamia ya watu wamejitolewa kutoa usaidizi pia.
Moto huo mkubwa umeharibu sehemu kubwa ya ya hifadhi ya Tsavo, ambayo iko Kusini Mashariki mwa Kenya.
Moto huo umehatarisha maisha ya wanyama pori na mimea.
Hifadhi hiyo ambayo ina mamia ya simba, tembo na vifaru, Imekuwa ikiwavutia watalii wengi wa kimataifa kila mwaka lakini sasa pameathirika na moto wakati ambao Kenya inakabiliana na janga la corona ambalo limesababisha taifa hilo kupoteza mabilioni ya dola katika pato la taifa.
Recent Comments