Bendera hii inawakilisha muungano ulioitwa Confederate States of America (CSA), umoja huu ulianzishwa mwaka 1861 baada ya majimbo 11 ya Marekani kuamua kujitenga katika nchi hiyo iliyokuwa na umri wa takribani miaka 85. Majimbo hayo ni Alabama, Arkansas, Florida, Georgia, Louisiana, Mississippi, North Carolina, South Carolina, Tennessee, Virginia na Texas.
Uasi huo wa majimbo 11 ulichochewa zaidi na kuchaguliwa kwa Abraham Lincoln kuwa rais wa marekani kipindi hicho ambapo, Rais Lincoln alikuwa na msimamo wa kusitishwa kwa biashara ya utumwa, huku majimbo hayo yalikuwa yanatetea vitendo hivyo.
Kukazuka vita kubwa kati ya majimbo hao na majeshi ya Marekani. Ni vita vilivyodumu kwa miaka 4, vikionekana kama vita kati ya watu weupe na watu weusi, kabla ya kumalizwa mwaka 1865, ikionekana kama ushindi dhidi ya utumwa na ubaguzi wa rangi.
Baada ya vita hiyo, kumekuwa na harakati za muda mrefu za kukabiliana na utumwa, kwa zaidi ya miaka 155 nchini Marekani, lakini harakati zinazoonekana kuwa tata, wamarekani wengi weupe, hasa wa Kaskazini mwa taifa hilo, wameonekana kutojitoa sana kupambana dhidi ya ubaguzi.
Kupigwa marufuku kwa bendera za”Confederate Flag’ na viashiria vyote vinavyoonekana kutukuza utumwa na ubaguzi wa rangi, vilianza kutoweka kidokigo ikiwemo makao makuu ya Bunge la Marekani, huku maeneo mengine mengi wakipiga marufuku.
Wachuuzi wa bendera walitangaza kutoziuza kutokana na namna zinavyochukuliwa, huku kifo cha mmarekani mweusi, George Floyd, kilichocheza zaidi hasira za kutokomezwa kwa viashiria vya ubaguzi ikiwemo bendera hizo
Ingawa ni zaidi ya miaka 150 sasa tangu majimbo hayo 11 yashindwe vita kutetea utumwa, bado bendera hiyo inaendelea kuigawa Marekani, lakini kuleta msigano pia hata nje ya taifa hilo hasa kwa watu weusi.
Watu wanaoonekana kuwa na bendera hizo katika himaya zao wanachukuliwa kama ni watu wanaotukuza vitendo vya utumwa na ubaguzi wa rangi. Kwa watu weusi, bendera hiyo inawapa hasira wakirejea mateso na maumivu ya utumwa na ubagunzi yaliyofanyika kwa miaka mingi wakati wa utumwa. Watu wengi weupe hasa nchini Marekani wanaopeperusha bendera hizo hukutana na mashambulizi ya mara kwa mara na wengine wakihukumiwa.
Lakini baadhi ya Wasanii weusi wamekuwa wakiitumia bebdera hii na kuwapelekea kuwa matatani na kufanya kazi zao kupata vipangizi hivi karibuni msanii wa Tanzania Diamond Platinumz ameingia kwenye sakata hilo baada ya kuonesha bendera ya confederate kwenye ngima yake ya Gidi na kupelekea kushambuliwa mitandaoni pia Kanye west na Ludacris walishawahi kuwekwa kitimoto kisa hii bendera
Recent Comments