Mwanamke amekuwa akichukuliwa kwa utofauti sana katika jamii mbalimbali ambpo baadhi ya jamii humuona kama mlezi tu wa familia, zingine kiumbe dhaifu, zingine humuona mwenye nguvu na wakutegemewa.
Kiukweli uelewa wa baadhi ya jamii bado mdogo sana juu ya mwanamke hali inayopelekea wadharauriwe na kunyanyaswa bila kutambua uhalisia na thamani ya mwanamke katika jamii.
Siyo kweli kwamba kuna mambo mwanamke hawezi kuyafanya na huku mwanaume anayafanya, ukweli ni kwamba wanawake wanaweza fanya kila kitu iwe kulima, kubeba mizigo, urubani unahodha kwa ufanisi muda mwingine kuliko hata wanaume hivyo si vyema kuweka mitazamo hasi juu ya mwanamke katika jamii.
Watu wanashindwa kuelewa kuwa kuna la Jinsi (sex) na jinsia (gender) ambapo jinsi ni maumbile tu huku jinsia huwa ni ya mwanaume na ya mwanamke ambapo hili hufanya watu waweke uthamani wa jinsia na jinsia na kufanya wanawake waonekane hawawezi baadhi ya mambo na kuwa chini ya wanaume.
Nikupe ukweli tu leo ni kwamba mwanamke si dhaifu hivyo basi anaweza fanya chochote wakati wowote na popote na ndiyo maana unaona baadhi yao wana mafanikio makubwa zaidi ya wanaume mfano mzuri samia Suluhu ambaye ni raisi Tanzania, queen Latipha tajiri marekani na wengine wengi tu, hivyo basi mwanamke apewe nafasi na siyo kudharaulika.
Recent Comments