Suala la kitambi au tumbo kubwa limekuwa mtambuka Sana Kwa sasa, suala hili limekuwa li kiwawazishwa watu wengi mno na kumpelekea mfadhaiko ubovu WA mahusiano na hata hatari katika afya. Kichwa ya kuwa suala hili ni Baya Kwa jamii nzima lakin wanawake wamekuwa ndiyo wahangavwakubwa WA suala hili la kitambo na hii ni Kwa sababu si kawaida wap kuwa na tumbo kubwa.
Sababu kubwa inayosababisha vitambi huwa ni uvivu na ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi ikiwemo nyama,chipsi Pia kuwa wavivu kufanya mazoezi.   Â
Je kitambi ni nini?
Kitambi ni mafuta yanayorundikana nyuma ya ngozi ya MTU hasa ya tumboni mafuta hayo huitwa viceral fat ambapo ni muhimu Kwa afya lakin yakizidi huwa na madhara Sana.
Jinsi ya Kuondokana na Kitambi
Kuna njia nyingi Sana za kuondoa kitambi lakin Leo nitakupa njia chache Tu kwaajili ya kuimarisha afya yako na kuepukana na adha ya kitambi.
1. Mazoezi Ya Viungo ;
Mazoezi nibkitu muhimu muno hivyo unaweza kufanya mazoezi ya aina nyingi ili kupunguza tumbo. Mazoezi yo yote ya nguvu yatapunguza mafuta ya mwili wako pamoja na mafuta ya ndani (visceral fat).
Mazoezi ya kadri ya dakika 30 mara tano kwa wiki yanafaa, kama vile kutembea, ili mradi unatoa jasho, yatakufanya uheme kwa haraka na kuongeza mapigo ya moyo wako.
Unaweza kupunguza muda kwa kufanya mazoezi ya nguvu zaidi kama jogging kwa dakika 20 mara nne kwa
2. Matumizi ya Chakula vyema;
Chakula ni kitu ambacho ndiyo chanzo kikubwa cha kasababisha kitambi japo kuna maandishi mengi mno kuhusu somo hili la kupunguza mafuta ya mwili kwa kuwa na mpango mzuri wa ulaji chakula. Kwa kifupi unahitaji kuzingatia yafuatayo:
-Kula mboga za majani kwa wingi sana kulijaza tumbo lako
-Kunywa maji mengi sana
-Weka chakula cha kukutia hamu mbali na nyumba yako
-Tafuta shughuli za kukufanya uwe busy kila wakati
-Kula kutoka kwenye sahani tu ukiwa umeketi mezani
-Kula milo yote, acha tabia ya kuruka milo.
3. Jipe Usingizi Wa Kutosha
Kupata usingizi kwa muda mzuri kumeonyesha kuwa na mchango katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika mwili wa binadamu. Katika utafiti mmoja, watu waliopata usingizi kwa saa 5 hadi 6 kwa siku katika kipindi cha miaka 5, walionyesha kuwa na mafuta mwilini kidogo zaidi ukilinganisha na wale waliopata usingizi kwa pungufu ya saa 5 kwa siku au wale waliolala kwa saa 8 au zaidi kwa siku.
4. Virutubishi
Kuna virutubishi ambavyo vimethibitika kusaidia kupunguza uzito wa mwili. Virutubishi vinafanya kazi vizuri ikiwa mwili utakuwa na kiwango kizuri cha madini ya calcium katika damu. Tafiti zimeonyesha kuwa asilimia moja ya madini ya calcium ndani ya mwili huwa katika mzunguko wa damu. Kiwango hiki cha calcium kikipungua, homoni ya parathyroid huzuia uvunjwaji wa mafuta katika mwili. Hivyo basi, kama kiwango cha calcium katika damu kitakuwa kimepungua, zoezi la kupunguza mafuta mwilini halitafanikiwa.
Naamini kupitia njia hizo utaona matokeo Bora na utaepuka kitambi.
@Ventas Malack
Recent Comments