Recent Comments

Jumbe toka kwa Mugabe kwa Ajiri ya Siku Kuu

By Baraka Bitariho Dec 20, 2023
Jumbe zenye maana toka kwa Mugabe. Je hizi jumbe zinakugusaje, zinasaidiaje jamii ama zinamaana gani? Tumia muda huu wa siku kuu kutafakari na uzitumie katika maisha yako popote dunian ulipo.

Pengine Jumbe toka kwa Rais wa zamini wa Zimbabwe, hayati Robert Mugabe zinaweza kugusa kila mtu popote alipo, awe mjini ama kijijini. Simamia.com na Ngaratv.com ikaonekana ni vyema zifike kwa walengwa.

Jumbe zenye maana toka kwa Mugabe.
Je hizi jumbe zinakugusaje, zinasaidiaje jamii ama zinamaana gani? Tumia muda huu wa siku kuu kutafakari na uzitumie katika maisha yako popote dunian ulipo.

Kumpongeza Mwanasiasa kwa kujenga Shule,Hospitali au Barabara kwa fedha za Umma ni sawa na kuishukuru Mashine ya ATB pale unapokwenda Benki kutoa Pesa. Hii Haina tofauti na kile kinachoshuhudiwa na Wana Ngara kumpongeza na kufagilia kwa Wanasiasa wanaowapa fedha kwa lengo la kutafuta Umaarufu na uungwaji mkono ili wawachague tena. WANANCHI wanatakiwa kutambua kuwa Pesa wanazopewa, mgoligoli na Gwagwa wanazonunuliwa ni Mshahara wao. Kuelekea Uchaguzi,Pesa zikija pigeni ila mjue kuwa ukichaguwa vibaya  malipo yake ni Miaka mitano tena mpaka Uchaguzi. Dawa ya Malaria ni chungu ila inaponya. Baadhi ya Wanasiasa hawapemdi kuambiwa Ukweli,wafike sehemu wawaambie ukweli Wananchi. Tafakari, Chukua na hatua.