Recent Comments

KABLA NA BAADA YA UHURU WA TANZANIA HAKUNA MAJI SAFI NA SALAMA NYAMAGOMA

By Mwafrika Aug 22, 2024
Exif_JPEG_420

Na mwafrika

Wananchiwa kata ya NYAMAGOMA iliyopo Wilayani Ngara wameiambia Simamia.com Kua wanashida ya maji safi na salama.

(Wananchi wakichota maji Kwenye karavati)

Wananchi hao wamesema maji wanayoyatumia ni chanzo Cha mto ambao unapita katika mabonde na ndio maji wanayolazimika kuyatumia kunywa hata kupikia wakati mwingine.

Wamesema katika mpaka wa Kijiji Cha murubanga na kumubuga ndipo maji yalipo ambapo Enzi hizo palikua Kambi ya wakimbizi kutoka Burundi na ndipo maji safi yalipo pale ila chakushangaza chanzo Cha maji kimepeleka Huduma Nyakahura huku wananchi hao wakikosa maji safi ili hali mradi Upo katani kwao.

Mashamba ya mbogamboga

Hata hivyo simamia.com imefanya utafiti mdogo juu ya maji wanayoyatumia wananchi hao na kuona uwepo wa hatari ya kupata maradhi mbalimbali ikiwemo Kansa na kipindupindu baada ya kuona baadhi ya maeneo yanapopita maji hayo Wananchi wamelima mbogamboga na mazao mengine na kuonesha wanatumia dawa za kupulizia wadudu na kurutubishia mazao jambo ambalo ni hatari Kwa watumiaji maji katika kata ya Nyamagoma Kijiji Cha Murubanga.

Haya ndio maji wanayoyatumia

Wananchi hao wameomba uongozi kuingilia Kati Ili kuwapa Wananchi huduma ya maji safi na salama Ili kuepusha madhara yayakayotokea Kwa matumizi ya maji yasiyo na vigezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *