Unapokuwa kijana kuingiza kipato ni suala muhimu sana maana maisha utengenezwa ujanani na kuenjoy unapopata nafasi ya kuishi uzeeni, watu wengi na vijana wengi hupata nafasi ya kufanya kazi na kwa sasa wengi hujiajiri lakini kipato hakikui na kubaki palepale na hali ileile kama walivyoanza. Sasa leo nakuletea mbinu hizi ambazo unaweza kuzitumia kuongezea kipato chako na kukikuza kiwe kikubwa kabisa.
A) Ongeza Ufanisi wa Kazi
Ili kuongezea unachokipata unatakiwa kuifanya kazi yako au biashara yako kwa ubora zaidi hii huambatanisha kuwahi kufika kazini kila siku za kazi na jioni kuchelewa kuondoka kazini kila siku za kazi na pia kujifunza zaidi juu ya kile unacho kifanya kiwe bora.
B) Matumizi sahihi ya Muda
Kiuhalisia muda ni mali hivyo basi ni muhimu kujishughulisha na jambo lolote ambalo litakuletea faida kwa kuzingatia muda ukipata oda fanya kwa muda sahihi, kuandaa biashara iwe kwa muda sahihi na mengineyo.
C) Ubunifu
Kitu kinachotofautisha biashara yako na zingine ni ubunifu hivyo basi kiwango cha ubunifu lazima kiongezeke cha uzalishaji binafsi, yaani kumiliki bidhaa zitokanazo na mikono yako pia zenye utofauti utaofanya watu waone utofauti wako ni muhimu.
D) Tanua biashara yako
Pia Ili kuhakikisha kuwa unaimarika kiuchumi ni lazima uimarishe uchumi wa biashara yako kwanza siyo kila siku upo na kiasi kilekile cha bidhaa na mtaji unatakiwa kukuza mtaji, na kutanua soko lako ili kupata faida zaidi.
E) Kutokata Tamaa
Ili kuhakikisha kuwa kazi unayo ifanya unaweza kuimudu vizuri, matatizo yanayo toke kazini kwako uyaone kama changamoto lazima uwe na uwezo wa kuzikabiri ili uweze kusonga mbele Kiuhalisia changamoto huumiza sana lakini hazina budi kuja hivyo basi pia wewe usiziogope na kukata tamaa zivae pambana nazo yaani usikate tamaa
Recent Comments