Recent Comments

KAMCHAPE (LAMBALAMBA) WAENDELEA KUCHONGANISHA JAMIMI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA.

By Mwafrika Sep 16, 2023

NA,MWANDISHI WETU.

Licha ya serikali kupitia Jeshi la polisi nchi Tanzania kupiga vita wanganga wa kienyeji Kamchape alimaarufu kama Lambalamba kupiga marufuku waganga hao kuendelea na shughuli zao za kuchapa wanao daiwa kuwa ni wwchawi bado ukanda wa ziwa Tanganyika waganga hao wanakaidi agizo hilo.

Aidha simamia.com imeshuhudia baadhi ya waganga wakiendesha zoezi hilo mkoani Kigoma katika maeneo ya vijijini pamoja na Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

Vilevile waganga hao uandaa makundi ya vijana ambayo hufanya kazi nyakati za usiku na kuweka vitu vinavyo ashiria uchawi katika makazi na mashamba ya watu ambapo waganga hao hufika katika maeneo hayo na kujifanya waonaji ambapo humdai kiasi cha fedha mmliliki wa eneo hilo anapo goma kutoa pesa hiyo hutishiwa kuwa baada ya kipindi fulani atakufa ama anaweza kupata madhara mbalimbali katika familia yake.

Hata hivyo simamia.com imeenda mbali zaidi na kuzungumza na baadhi ya wanachi ambao wamegoma kabisa kutajwa majina yao wala kupigwa picha ambao mmoja wao tumembatiza jina la Hamis amesema kuwa hivi karibuni waganga hao wakifika nyumbani kwake nakwambia kuwa Kuna uchawi ulikimbia kutoka kwa mtu mwingine na kuingia kwenye Jiko lake (Nyumba anayo tumia kupika chakula) hivyo basi atoe kiasi cha pesa pamoja na Kuku ili wauondoe uchawi huo, baada ya kugoma kufuata maelekezo hayo walimtishia kuwa atakufa.

Ameendelea kwakusema kuwa suala hilo limemchonganisha na familia yake pamoja na jamii nzima ambapo baadhi yao humchukulia kama ni mchawi kweli na wakati hana historia hiyo ambapo kwasasa ana umri wa Miaka inayo kadiriwa kati ya Miaka 70 mpaka 80.

Pia simamia.com imebaini kuwa kuna baadhi ya wananchi wanaamini himani hiyo potofu ambapo hulipa pesa kwajili ya shughuli hizo humu baadhi ya viongozi wakishiriki katika zoezi hilo.

Ifahamimie kuwa Kamchape (Lambalamba ) ni Imani Potofu na Uchonganishi kwa jamii pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu na udharirishaji kwani hata serikali haihararishi uchawi.

Lakini simamia.com inahiji suala la waganga hao kuendelea kupewa ushirikiano na viongozi wa serikali na hata kupewa ulinzi hasa katika wilaya ya Tanganyika hii inamanisha kuwa huko kuna serikali nyingina?

Hata hivyo simamia.com imeweka kambi katika wilaya ya Tanganyika na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kigoma ambapo matukio haya yanaendelea tutakujuza kila kinacho endelea huku endelea kufuatilia simamia.com kila siku na simamia tv YouTube.