KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI ZAPAMBA MOTO KAMWENE (W) KILOMBERO.
Na Musa Mathias.
Email. Mussamathias573@gmail.com
Morogoro
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Morogoro wamefika kitongoji cha Mjimwema kata ya Kamwene wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kwa lengo la kumnadi mgombea nafasi ya Udiwani wa kata ya Kamwene kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi anayefahamika kwa jina la Gervas Zugumbwa.
MMgombea huyo kupitia tiketi ya CCM Ndugu Gervas Zugumbwa amenadiwa vema na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiwemo wa Mkoa, Wilaya na Kata lengo ikiwa ni kuhakikisha wanaongezaushawisho utakaopelekea kushinda uchaguzi mdogo ambao ulitangazwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi wiki chache zilizopita.
Mwisho.
Recent Comments