Kampuni moja ya data ya mitandaoni iliomfanyia kazi Donald Trump na ambayo ilitumika katika kampeni za Brexit sasa imeripotiwa kumfanyia kazi rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Lengo la Cambridge Analytica ni wazi. Katika Mtandao wake kampuni hiyo inasema inatumia data kubadili tabia ya wateja wake.
Kampuni hiyo iliokodishwa na kundi la kampeni za rais Trump imepongezwa kwa ushindi wa rais huyo.
Kampuni hiyo inanunua na kukusanya data kuhusu wapiga kura ikiwemo historia ya utumizi wao wa mtandao, mahali walipo pamoja na ‘Likes’ zao {wanachopenda} katika mtandao wa facebook.
Katika mtandao wake, Cambridge Analytica inadai kukusanya maeneo 5,000 ya data miongoni mwa wapiga kura milioni 320 wa Marekani.
Zinapochanganywa pamoja na utafiti unaofanywa , Cambridge Analytica inaweza kutumia data hiyo kutoa ujumbe muhimu kwa wapiga kura.
Kwa sasa Cambridge Analytica inafanya kazi Kenya , ikisaidia juhudi za kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru kenyatta…
Kwa jina anaitwa Shaban Rashid Said Kisleu na ni mhariri hapa Simamia Media Group.
Natumaini mtafurahishwa na yake nitakayowaletea na mtaendelea kufatilia mitandao wa Simamia.com
Kumfikia, tuma email SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments