Na,Muhngo Mwemezi-KIBONDO
Licha ya mwitikio mzuri wa Kilimo cha Alizeti Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma,bado wanakabiliwa na gharama kubwa ya pembejeo za Kilimo Pamoja Mbegu ambapo kwa kilo moja ya mbegu ya OPV kilo moja ni shilingi Sh 5 elfu na Chotara ni Sh 22 elfu
Akiongea kwenye Kikao maalum kilichoka kwa lengo la kujadili maendeleo ya zao la Alzeti Afisa Kilimo wilayani humo Salvatory Kaimu amesema kwa Wananchi wa wilaya hiyo ni zao geni na wakulima walioitikia kwa awali Idadi yao ni 1046 na hekali zilizolimwa ni 1,183 ikiwa lengo ni wakulima kujiendesha wenyewe hapo baadae, badala ya kuendelea kuitegemea  Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo inayosaidia kwa sasa
ââMaendeleo ya kilimo hicho ni mazuri, Wakulima wamejitokeza wa kiwango kinachoridhisha kutokana na kilimo cha Alizeti kuwa mara ya kwanza kulimwa kwa lengo la Biashara na mategemeo yetu hapo baadae ni kulima hekali 5000 maana tunatarajia mavuno yatakuwa mazuri kutokana na wale waliolima kwa mara ya kwanza, zao hilo kuonyesha dalili nzuri japo mavuno hayajaanza alisema Sarvatory
Zao la Alizeti ni zao jipya ambalo limeanzishwa kwa lengo la kukuza uchumi wa wilaya ya Kibondo kutokana na kutokuwa na mazao rasmi ya kibiashara japo kilimo kinachotegewa kama Mhogo, Mahindi na  Maharage mazao hayo yamekuwa yakitumika kwa chakula na Biashara ambapo kwa sasa limeanzishwa na zao la Korosho, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibondo Diocles Lutema amesema kinachotakiwa ili mafanikio yaweze kuwepo katika secta ya Kilimo, ni maafisa Ugani kutimiza wajibu wao kwa kutoa ushauri kwa Wakulima
Kikao hicho cha Mkakati wa kuboresha kilimo cha Alizeti kilihusisha wataalam wa Kilimo ambapo wamesema kwa sasa bado baadhi ya Wakulima wanahitaji msaada juu ya kilimo hicho Alizeti na Mengine hasa kwa mazao mageni Kama Korosho na Alizeti
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura amesema bado hamasa inahitajika kwa wananchi waweze kujitokeza, na iwapo kama watakubali hasa kwa Makundi ya Vijana wataweze kuinua uchumi wao mmojammoja kutokana na mazao ya Korosho na Alizeti kuwa na Masoko ya uhakika na yenye bei zinazoridhisha kulingana na Garama anazokuwa ametumia Mkulima
Kwa upande wao baadhi ya Wakulima ambao wameitikia kilimo cha Alizeti ambao ni Proches Kitaronja na Kened Sarundali wamesema Kilimo hicho kimekuwa na wepesi kutokana namaanadali ya mashamba ambayo wameyatumia baada ya msimu wa mavuno uliopita na kueleza wasiwasi wao huenda kuwawepo changamoto ya Mashine za kuchatia Alizeti hapo baadae
âTumejaribu kilimo hiki lakini mashaka yangu ni viwanda kwa ajili ya kuchakata ili kupata mafuta na kupata masoko  tunaiomba serikali kulitazama kwa jicho la pekee suala la upatikanaji wa mashine hizo wakulima wasije wakakata tamaa amesema Sarundale
Mwisho
Recent Comments