Katika pitapita zangu nimekutana na Mashamba ya mazao kama viazi,maharage na mazao mengineo,kwa sasa tunatambua tupo katika kipindi cha kiangazi hivyo ili ufanye shughuli ya kilimo lazima utumie umwagiliaji au kuruhusu maji kupita kwenye matuta(mifereji)kupitia chanzo cha maji.
Usishangae kwa msimu huu wa kiangazi ukikutana na mahindi hasa ya kuchoma maana kuna mabonde ambayo mito midogo imepita na wananchi wamejiongeza kulima kwa kururhusu maji kuingia kwenye mazao.
Simamia.com tunawapongeza sana wananchi wanaoishi kata ya kabanga kwa kuonyesha namna gani wanaweza kutumia fursa iliyopo kuwapatia chakula na hata kipato kwa kuuza mazao.
Na hili liwe jambo la kuigwa kwa watu wengine ambao wanaishi karibu na mito midogo huku wakiacha maji yaende bure bila kuyafanyia kazi huku wengine wakichukulia kana kero kwao hasa pale kipindi maji yanapokuwa mengi zaidi na kuzuia hata njia zao.
Niwaulize tu hivi kwanini msijiongeze na kufurahia neema ya Mungu maana wengine hawajapata hiyo fursa na maeneo yao asilimia kubwa ardhi ni jangwa na wanatamani hata wapate maji ya kidimbwi.
Ok basi hata kama hamna pesa kwa mtu mmoja mmoja nawashauri unganeni na mjikusanye hata mnunue mota ya kuendesha hayo maji ili hata aliyopo mbali na maji aweze kumwagilia maana Dunia ya sasa imebadilika na hata majira bayo yamebadili.
Mungu ametupa akili na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kwa kutumia nguvu ama uwezo sasa kwanini titegemee mvua kila siku?ok na nyie serikali kwanini hamtoi elimu kwa watu kuhusu kilimo cha umwagiliaji na Dunia inavyoenda kwa sasa?
Sawa tukisema tunaambiwa tunaongea kwakua hatujawahi kuongoza hata kondoo ndio hatukatai ila nanyi mjitazame kwa upana ili mkwamue wananchi wenu kiuchumi na kuongeza pato taifa pamoja na wananchi kiujumla.
Recent Comments