Recent Comments

Uchaguzi Marekani 2020: Hasimu wa Rais Donald Trump, Joe Biden amesema ameiweka Marekani gizani kwa muda mrefu

By ObyMack David Aug 21, 2020
Makamu wa rais wa zamani, Joe Biden amesema kuwa hasimu wake amesabisha '' hasira nyingi, uoga mwingi na mgawanyiko mkubwa

Joe Biden amesema kuwa Rais wa Marekani Donald Trump ”ameiweka Marekani kwenye giza kwa muda mrefu” alipozungumza wakati akikubali kuteuliwa kwake kupeperusha bendera ya chama cha Democratic kuelekea Ikulu.

Makamu wa rais wa zamani amesema kuwa hasimu wake amesababisha ” hasira nyingi, uoga mwingi na mgawanyiko mkubwa”.

Hotuba ya Biden ni kilele cha kazi ya kisiasa iliyochukua karibu nusu karne.

Anaelekea kwenye kampeni za uchaguzi mkuu akiwa anaongoza kwa kura za maoni dhidi ya Rais Trump

Lakini zikiwa zimesalia siku 75 kabla ya uchaguzi, Rais wa Republican ana muda mwingi wa kupunguza tofauti ya kura hiyo.

Joe Biden amewataka Wamarekani kufanya maamuzi sahihi kuelekea miaka minne mingine

Akiongea kwenye hafla mjini Wilmington, Delaware, Biden, 77, amesema ”sasa hivi hapa, ninawaahidi, ikiwa mnaniamini kwa kunipa jukumu hili la urais, nitahakikisha sisi tunakuwa bora zaidi.

”Nitakuwa mshirika wa nuru, na si giza.

”Ni wakati wetu, wa kuwa pamoja na kuhakikisha hatufanyi makosa, kwa kuungana tunaweza na tutapambana na msimu huu wa giza Marekani.

”Tutachagua matumaini dhidi ya hofu, uhalisia kuliko mambo ya kufikirika, haki kuliko upendeleo.”

”Tunaweza kuchagua njia ya kuwa na hasira zaidi, isiyo na matumaini, iliyogawanyika zaidi,” alisema.

”Au, tunaweza kuchagua njia tofauti na wote kwa pamoja tukatumia fursa hii ili kupona, kufanya mabadiliko, kuungana. Njia ya matumaini na nuru.”

”Huu ni uchaguzi wa kubadili maisha. Hii itatupa mwanga wa namna Marekani itakavyokuwa kwa muda mrefu.”

Aliendelea: ” Tunachokijua kuhusu rais huyu ni kuwa ikiwa atapatiwa miaka mingine minne, atakuwa jinsi alivyokuwa miaka minne iiyopita.

”Rais ambaye hawajibiki, ambaye anakataa kuongoza, anayewalaumu wengine, anawafunika madikteta na kuchochea miale ya chuki na mgawanyiko.

”Ataamka kila siku asubuhi akiamini kuwa kazi ni kumhusu yeye na si ninyi.

”Je hii ni Marekani mnayoitaka kwa ajili yenu, familia zenu na watoto wenu?”

Hotuba yake mubashara imetamatisha siku nne za mkutano wa Democratic

Wazungumzaji waliozungumza kwenye mkuano siku tatu zilizopita wamemkosoa Trump kuwa mtu asiyemudu kazi yake, mbinafsi, na hatari wa demokrasia.

Presentational grey line