Recent Comments

KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, DC SAME ATETA NA WAZEE.

By Mussa Mathias Aug 27, 2024
Picha ikionesha mmoja kati ya wazee akieleza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Same.

KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, DC SAME ATETA NA WAZEE.

Wazee Wilayani Same wametakiwa kukemea vijana wao kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kujiepusha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa kushinikiza wagombea ili wawachague na badala yake washiriki kikamirifu kuchagua viongozi bora na waadilifu watakao simamia vyema fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa na Mhe Rais Dkt. Samia kwa wananchi wake.

Picha ikionesha mmoja kati ya wazee akieleza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Same.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni wakati akifungua kikao maalumu kilichoandaliwa na Diwani wa Kata ya Same kwa lengo la kuwaeleza wazee hao masuala ya uchaguzi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia amefanya Kata na Wilaya ya Same.

“Jambo jema na la faraja kwetu wakazi wa Same ni kuona namna miradi ambayo tumepatiwa fedha na Rais Dkt. Samia inavyosaidia kubadili uchumi wa Wilaya yetu lakini pia mwananchi mmoja mmoja, katika hili kwakweli mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Same namshukuru sana mama Samia Same yetu sasa inazidi kusonga mbele kwa kasi”. Alisema DC Kasilda.

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Aidha amesema kwa kutambua mchango wa wazee wa Same kwenye suala la uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba0 27 mwaka huu 2024, amesisitiza pia wazee hao kukaa na familia zao kuwaeleza habari njema juu ya umuhimu wa uchaguzi huu ambao ndiyo unatoa dira ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *