Na kabanga ni miongoni mwa kata zinazopatikana katika wilaya ya ngara na iliyobarikiwa kuwa na hadhi ya Boda(kobero)kati ya Tanzania (nzaza)na kobero Burundi.
Licha ya uwepo wa Boda hiyo inasadikika kata ya kabanga ni miongoni mwa sehemu inayokusanya mapato mengi katika wilaya ya ngara lakini kimaendeleo bado yanasonga kwa mwendo wa kobe.
Mwandishi wetu siku ya tarehe 23/8/2023 alitembelea sehemu moja ya kituo cha kutolea huduma ya maji(binafsi)katika msikiti uliopo maeneo ya karibu na egesho la magari(parking)na kushuhudia rundown la watu na foleni ya madumu ya maji.
Hii sio mara moja ni mwendelezo wa maisha yao japo kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeliona hili kwa kuleta mradi mkubwa wa maji ambao ujenzi wake ulianza mapema mwaka wa jana ila mpaka sasa hakuna harufu nzuri ya kupata maji hivi karibuni.
Kwanza pongezi ziende kwa viongozi wa wilaya ya ngara na watu wa idara ya maji Ruwasa wilayani kwa kuahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Kagera kuwa ifikapo tarehe 30 mwezi wa 8 maji yatakua yametoka na kupitia Simamia.com ilikuwepo kwenye usikivu wa ahadi hiyo na kuwataka viongozi walete furaha tele kwa wananchi wao.
Andiko hili ni katika hali ya kuona namna gani wanachi hao wamekuwa wakitaabika na wakiongea Simamia.com bila kutaka kujulikana kwa nyakati mbalimbali wamesema wanateseka na wanaiomba serikali iangalie jambo hili kwa jicho pana ili wananchi waache kutegemea mvua na badala yake kodi zao zifanye kazi.
Ikumbukwe kabanga kuna mradi mkubwa ambao umejengwa pale shule ya sekondari ambao utaweza kuhudumia kijiji cha kabanga na vitongoji vyake pia mradi huo ambao unagharimu takribani Million940+ ambao tayar vituo vimewekwa ila kuanzia tarehe 30 kwa mujibu wa meneja Ruwasa ngara maji yatakua tayari kuwafikia wananchi.
Recent Comments