Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amefunguka kuwa hakuna mtu anayepinga ulindwaji wa rasilimali za nchi hii na kudai labda mwendawazimu ndiye anayeweza kupinga, na kuongeza kuwa shida ipo kwenye namna ya ulindaji wa rasilimali hizo.
Lema alisema hayo jana bungeni kwamba nchi saizi imeingia kwenye mgogoro na mgodi wa ACACIA na kudai, mgogoro huo unakwenda kuvunja imani na moyo wa wawekezaji wengi kuja kuwekeza katika nchi hii jambo ambalo linaweza kuipelekea nchi ya Tanzania mbele ya safari kuwa kama Zimbabwe.
“Hatua ya kulinda rasilimali za nchi hii ni mtu mwendawazimu anayeweza asipongeze, lakini namna gani unalinda rasilimali za nchi hii inaweza ikaigharimu taifa hili na kuliingiza kwenye matokeo mengi, Mh Mwenyekiti leo taifa hili wote tunafahamu kwamba nchi hii ina mgogoro na ACACIA Mining, mgogoro huo unajenga hisia na sifa za kisiasa ndani ya nchi lakini sura ya pili ya mgogoro huu unakwenda kabisa kuvunja imani na moyo wa wawekezaji kuja kuwekeza ndani ya nchi hii” – alisema Lema
“Mwenyekiti siyo tu ACACIA ukiangalia ardhi kwenye wizara ya Lukuvi imekuwa ni sifa kunyang’anya watu ardhi, imekuwa ni sifa kunyang’anya wawekezaji ardhi jambo hili mbele ya safari litaifanya taifa hili liende likawe kama Zimbabwe, siasa na biashara ni vitu vinavyofanana na mwanasiasa makini ni yule atakayejua maana ya uchumi, hawa wananchi leo wanaoshangilia baada ya miezi miwili mitatu watakosa chakula, wakikosa chakula itakuwa raisi kuingia barabarani” -Godbless Lema
Recent Comments