Habari za muda msomaji, naamini mambo ni mujarabu. Leo nataka tuongelee suala la mapishi ya mke kwa mumewe mwanamke unatakiwa kujiuliza Kwa nini mumeo apikiwe na kimada wakati wewe upo? si vyema sana mwanamke kupika kawaida hakuna limbwata zuri kwa mwanaume kama mapishi yako, mpaka akukumbuke muda wote hata ukitoka kwa kuwa una pishi zuri.
Kwa miaka ya sasa wanawake wengi si wazuri kwenye mapishi kwakuwa wengi husoma shule za bweni hivyo hawajifunzi vizuri kupika kutokana kutopata wasaa wa kupika.
Kiujumla wanaume hupenda kupikiwa vizurii na ratiba ya chakula kama ilivyo kwa mtoto mdogo ndipo avutiwe na mwanamke wake.
Mwanaume anahitaji kula mlo ulio kamili kila idara ili kila anapokwenda awe anakumbuka mlo huo asiwaze kwingine hata mgahawani akila akumbuke chakula cha mkewe ambapo utumie viungo vizuri na vyenye harufu nzuri ili kuvutia zaidi.
Kiujumla mwanamke amshauri mumewe ale nini na faida za chakula hicho pia ajifikirishe chakula kipi ampikie kuanzia kifungua kinywa mpaka cha usiku.
Hata kama una mfanyakazi jitahidi siyo milo yote apike mfanyakazi kwa siku nzima milo mingine pika mwenyewe maaana ina nafasi kubwa kwa ndoa yenu.
0Kumbuka kuna faida sana ya mwanamke kumpikia mume ambapo kubwa ni kumuimarisha kiafya pia kumsaidia kuwa shupavu kitandani kwa kumpa vyakula vyenye tija zaidi kuliko vyakula hatarishi.
Tafadhali Mwanamke kama hujui kupika jifunze mapema, tafuta hata mafunzo ya mitandaoni, soma majarida ya mapishi pia tazama vipindi vya mapishi au tafuta wanawake wanaopika vizuri wakufundishe mapishi ndiyo limbwata kuu kwa mume na siyo waganga kwani dawa zikiisha atarudi palepale lakini mapishi ndiyo kitu maana ndiyo humvutia zaidi kuwa na wewe changamka usiibiwe wewe.
By Ventas Malakalinga
Recent Comments