Mpuuzeni! Yako mambo anaweza kutuyumbisha kwa muda kwa sababu anatumwa. Lakini yako mambo hawezi kutuyumbisha na hawezi kufanikiwa hata kama DOLA nzima inamsimamia. Mojawapo ya mambo aliyoshindwa ni kuendelea kuiba pesa za Ruzuku kwa kushikiliana na Msajili. Jambo la Pili atakaloshindwa ni hili la kukaa na wahuni wenzake na kujiita BARAZA KUU kisha eti kutangaza anawafukuza “Wabunge wa Viti Maalum”. Yani mtu asiye Mwanachama (alishafukuzwa) ati anatumiwa na dola kutoa matamko ya kipuuzi kwamba amewafukuza Wabunge. Wabunge ambao tuliwapigania mwaka 2015 yeye akiwa nchini Rwanda alikopelekwa na JK na Dk. Dau wa NSSF. Kura tulizopata majimboni sisi tuliopigana ndizo zimetupatia Wabunge wa Viti Maalum na hiyo Ruzuku.
Nawaomba wanachama wawe watulivu, amefikia kiwango cha juu cha kuchanganyikiwa na hatafanikiwa. #Mtatiro J.
Endelea kuifuatilia simamia.com penye Ukwelii na Uhakika siku zoote.
Kwa jina anaitwa Shaban Rashid Said Kisleu na ni mhariri hapa Simamia Media Group.
Natumaini mtafurahishwa na yake nitakayowaletea na mtaendelea kufatilia mitandao wa Simamia.com
Kumfikia, tuma email SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments