MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema Rais Jakaya Kikwete anapaswa kutangaza msimamo wake iwapo yuko tayari kukabidhi serikali kwa wapinzani iwapo watashinda uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu. Anaandika Pendo Omary ⦠(endelea).
â
Lissu ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam, mbele ya mgombea urais anayewakilisha UKAWA, Edward Lowassa.
UKAWA ni Umoja wa Katiba ya Wananchi ulioundwa na vyama vinne ambavyo ni Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na National League for Democracy (NLD).
Lissu amesema iwapo Rais Kikwete hatatoa msimamo kuhusu utayari wa kukabidhi serikali kupisha UKAWA, wao watampeleka Lowassa Ikulu kwa nguvu ya umma.
âMabadiliko ni pamoja na Katiba mpya, jambo la kwanza kulifanya iwapo tutaandika Katiba mpya, tumemuomba Rais Kikwete atueleze utaratibu wa kukabidhi serikali ukoje na asisingizie kuwa halipo kwenye Katiba.
â⦠Na kama (CCM) hawapo tayari kukabidhi madaraka sisi tutampeleka Lowassa Ikulu kwa nguvu ya Umma,â amesema Lissu ambaye naye anagombea ubunge jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida.
Mgombea ubunge jimbo la Kawe ambaye anawakilisha UKAWA kupitia Chadema, Halima Mdee, amesema âTuwaambie Tume ya Taifa ya Uchaguzi tunataka madaftari ya walioandikishwa kupiga kura kwenye kila kituo kilichotumika kuandikisha wananchi.â
âMamilioni ya Watanzania hawana uhakika kama siku ya kupiga kura majina yao yatakuwepo. Tunajua CCM wameandaa kadi feki nyingi sana za kupigia kura. NEC wasipofanya hivyo tutaandamana mdogomdogo hadi Ikulu,â amesema Mdee.
Mdee ambaye anatetea kiti hicho alichoingia baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010, aliombewa kura na Lowassa akimsifia kuwa ni mbunge mchapa kazi hodari.
Mwenyekiti wa muda wa CUF, Twaha Taslima ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, amesema ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliomfanya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuridhia kuanzishwa vyama vya upinzani nchini.
Taslima ambaye kitaaluma ni mwanasheria na wakili katika Mahakama Kuu, amesisitiza kuwa bila ya upinzani imara nje ya CCM, chama hicho kitaendelea kutawala milele na ubovu wake.
âNilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuongoza nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake,â amesema wakili Taslima akinukuuu maandishi ya Mwalimu Nyerere katika kitabu cha alichokiita âUongozi wetu na Hatima ya Tanzaniaâ ukurasa wa 66.
OP MwananchiOnline
Recent Comments