MGOMBEA urais anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa amepiga kampeni ya kuomba ridhaa ya Watanzania majimbo ya Temeke na Segerea, mkoani Dar es Salaam.
Baadaye alikuwa ametarajia kufanya mkutano mkubwa ndani ya majimbo ya Ubungo eneo la Sinza, na Kawe, kwenye viwanja vya Tanganyika Packers. Anaandika Charles William ⦠(endelea).
â
Lowassa aliingia viwanja vya Temeke Mwembe Yanga saa 11:20 asubuhi kwa msafara uliomhusisha pia Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Mbunge aliyemaliza muda, Rajabu Mbarouk, Meneja wa Kampeni yake, John Mrema na kada wa Ukawa, Richard Tambwe Hiza.
Kwenye mkutano wa jimboni Temeke, Lowassa alishuhudia mgombea ubunge wa jimbo hilo anayewakilisha UKAWA, Abdallah Mtolea ambaye ni mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) akiomba kura kwa wananchi.
Hiza alianza kuhutubia akitaka Watanzania wamchague Lowassa kuwa rais badala ya kuchagua mtunisha misuli na mbeba vyuma akimaanisha Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
âDuniani kote urais sio kazi ya kutunisha misuli, kupiga pushups, kurukaruka wala kupiga misamba. Sasa CCM wametuletea mtu wa aina hii wanafikiri sisi ni wajâ¦? Uongozi ni kupangilia mambo na utulivu wa akili ndio maana mnaona Papa (Kiongozi wa Kanisa Katoliki) anaongoza Wakatoliki dunia nzima lakini sio mpiga pushups wala mtunisha misuli,â alieleza Hiza.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye aliwataka Watanzania kuipumzisha CCM kwani hata mgombea wake, Dk. Magufuli ameshakiri chama hicho ni kitanda chenye kunguni.
âMsiogope kuipumzisha CCM, Magufuli anapita akiwaomba Watanzania wasikichome moto kitanda chenye kunguni, mimi nasema hatutakiwi kulalia tena kitanda hicho tukitupe porini,â amesema Sumaye ambaye alihama CCM mwishoni mwa mwezi Agosti akisema kimeacha asili zake.
Akizungumza, Lowassa alisema anataka ridhaa ya Watanzania awe rais na ni muhimu akapewa na mbunge wa Ukawa jimboni Temeke ili kukamilisha safu ya utendaji kazi.
âDunia imebadilika sana, elimu ndio itakayotusaidia kupata rasilimali watu wa kuendesha viwanda, kujiajiri, kuimarisha sekta ya afya. Mimi nauchukia umasikini na nafahamu hatua muhimu ya kuuondoa ni kuhakikisha tunatoa elimu bora na bure ili watoto wa masikini waende shule bila ya bughudha,â amesema.
Kampeni Meneja Mrema aliwataka wakazi wa Temeke kusoma vizuri tuhuma za ufisadi ambazo anahusishwa Lowassa tangu zilipotoka mwaka 2007 na CHADEMA kwani mara zote walikuwa wakimnyooshea kidole kwa misingi ya uwajibikaji wa pamoja kama mtendaji mkuu wa serikali lakini âhakuna mahali yeye binafsi waliwahi kumtaja kuchukua fedha au kuiba.â
âSeptemba 15, 2007 hapahapa tulitaja orodha ya mafisadi 11, tukaelezea kila mmoja tuhuma zake na tuliliweka jina la Lowassa kama namba 9 kwa sababu ya uwajibikaji wa pamoja. Huwezi kumtuhumu rais na mawaziri wake ukamuacha waziri mkuu, someni orodha hiyo mtaona tumeelezea tuhuma za (Rais Jakaya) Kikwete kurasa 4, (Andrew) Chenge kurasa 9, lakini Lowassa mistari mitatu kwa kuwa hatukupata ushahidi wa moja kwa moja kumbana.â
Lowassa alijiuzulu 8 Februari 2008 kwa shinikizo la Bunge lilipokamilisha mjadala wa ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya mkataba wa kufua umeme ambao serikali iliutoa kwa kampuni ya Richmond Development Company (RDC) iliyobainika haikuwa na uwezo wa kifedha wala vifaa.
Tangu wakati huo, serikali haikumshitaki Lowassa zaidi ya kumsakizia ndani ya chama kwa kumuita gamba ambalo hata hivyo CCM walishindwa kulivua.
Lowassa aliondoka Temeke saa 6.30 mchana na kwenda moja kwa moja viwanja vya Tabata Liwiti, ndani ya jimbo la Segerea ambako alimnadi mgombea ubunge jimbo hilo, Julius Mtatiro (CUF) anayewakilisha UKAWA.
Akiwa Tabata Liwiti, Lowassa alitaka wananchi wamchague kwa kura nyingi ili aje kuwapa faida ya kutatuliwa shida zao mbalimbali kwa kuwa ana dhamira hiyo na uwezo anao.
OP MwananchiOnline
Recent Comments