Vijana wengi waliongea na gazeti la Simamia.com hawakupenda majina yao kutajwa bado wana wasisi wasi na mgombea urais kupitia tiketi ya chama cha Chadema. Kwa hiyo maneno yao yaneandikwa kwenye nafsi ya kwanza ili ujumbe wao ujulikane bila wao kutambulika.
Tusipoteze muda kuongelea tusiyoyajua. Wengi wetu ni watoto wa ’80. Hatujui kitu na ndio wengi wetu hatuna kazi kutokana na hali yenyewe ya uchumu. Hata kama wote tungekuwa tuna elimu hapa Tanzania hakuna kazi za kutosha ambapo wote tungekua tunafanya kazi ofosini. Hata kama tungekua tumesoma bado tungekua mitaani kujitafutia liziki wenyewe. Wangapi leo wana elimu nzuri na vyeti kutoka shule za maana na hawana kazi?
Na pia kuna wengi hata form four hawajamaliza na wanahela zao na labda wanaajiri wale waliokuwa na elimu kubwa.
Tunashuhudia uigizaji mwingi wa Lowassa na tunamaswali mengi ambayo hatujajibiwa. Matendo ya Lowassa na Ukawa ndio yanatuacha na maswali mengi.
Lowassa amekua kwenye siasa kabla sijazaliwa. Lowassa anamalia kuomba kura kutoka kwa vijana na sio wazee. Hao wanaomjua anajua wanamfahmu vizuri na hawarudhishwi na historia yake ama?
Kama hata wale aliofanya nao kazi hawakuona Lowassa anafaa kuta hata kwenye tano bora za CCM, hapo lazima niziulize. Kwa nini nikubaliane na uigizwaji anaoufanya sasa hivi?
Kama haaminiwi na aliofanya kazi muda wote ni lazima wanajuamaovu alioyafanya. Aliaminiwa na wananchi aende bungeni kuwawakilisha. Yeye alienda kwenye siasa kujitajirisha. Amezichota sana hizo pesa kwa zaidi ya miaka 25 halafu leo anakuja kutucheka sisi wananchi eti tupo maskini sana. Tulimkabidhi imani na maisha yetu akatulinde na kutuwakilisha. Yeye baada ya kututumikia alienda kujitajirisha. Leo nchi ipo nyuma kiuchumi halafu anasingizia CCM. Je yeye hakuwa kwenye hiyo CCM muda wote huowakati uchumi unaharibiwa? Kwa hiyo yeye imemchukua miaka zaidi ya 25 kujishibisha hlafu leo anatufanya sisi wajinga nakusema CCM ndio imetufirisi. Yeye alikua mmoja wapo, alichota za kutosha na akatumia jasho letu kusomesha watoto na kunufaisha familia yake huku sisi tunaumizwa na maisha magumu ya umasikini. Umasikini unaotuumiza leo ulisababishwa namatendo yake akiwa CCM. Alikia mmojawapo na hawezi kutuletea sanaa na kudai asingeweza kufanya lolote akiwa CCM. Mbona yeye ndie tajiri kuliko wanaCCM wengine. Unataka kutwambia alikua hawezi kutusaidia ila anaweza kuzichota na kujitajirisha tu. Kwani tulimtuma Bubgeni akajitajirishe yeye?
Pili kama mtu niliesomea sheria, najiuliza ni kwa nini Lowassa hataki kuongea sana. Anaongea machache kidogo kila anapopewa uwanja wa kuongea? Kutoongea sana kunamsaidia asiseme mengi maana anaweza kujikwaa.
Hayo ni machache ambayo yanaitaji ufafanuzi.
Bado wengi tupo tupu tu, hatujui kama kura kwejye chumba cha kura tutapoteza kura zetu na kumpa Lowassa.
Atadanganya baadhi ya wale waliozaliwa baada ya mwaka 80 ambao hawajui kitu. Wale wengine watatumia akili kutafari kabla ya kupiga kura. Kupiga kura ni haki tuipatao mara moja katika mika mitano. Tuaipoteze hii haki kwa kupigia yule mtu asiekuwa safi. Hisgoriabya mtu ndio kielelezi cha kumbania mgombea.
Asante sana,
Habari hizi zimepokelewa na kuandikwa na mwandishi wetu,
Baraka Bitariho
Www.simamia.com
Recent Comments