Hodi hodi Ngara, huu ni msimu wa Sikukuu na Kamera nene ya mwanahabari wetu Kufuri ipo Ngara kusherehekea Krismasi na Mwaka mpya.
Ingawa internet na njia za mawasiliano bado ni kitendawili na dawa kwa sikio lililoziba, na andika makala hii leo nikitokea hapa kata ya Ntobeye.
Richa ya changamoto zilizopo, na amini kuwa huu ni ujio wa mkombozi wa habari za Ngara kupitia mtamdao makini wa www.simamia.com na Simamia TV
Safari ya Dar es salaam hadi Kabanga ilikuwa nzuri na inayotafakarisha sana. Camera yetu imeshuhudia magari mengi na ya kisasa yakiingia Wilayani Ngara
Ni wananchi wanaoishi Mikoani na kwenye majini ambao wanakimbizana kwenda Ngara kusherehekea sikuluu
Kwa jicho lingine Ni kama mfugaji wa kuku,ambaye hajui kuku wake asubuhi wakiamka wanakwenda wapi kutafuta chakula na usiku wanarudi kulala
Kwa sababu wengi wanaenda nyumbani kwao wakati waaikukuu tu. sikukuu zikiisha msafara wa magari hayo yataanza tena safari kurejea mijini.
Yaaani yale ma Tesla, VX,Prado,Benz, Harrie,na mengine mazuri yote tuliyozoea kuyaona mijini,Mikoani na kwenye majiji kama Dar es salaam,Arusha,Mwanza,na miji mingine mikubwa ya Mbeya,Tanga sasa yanapishana Ngara.
Wanaoitwa mabosi huko mikoani sasa wanashindana kwenye Baa na Club mjini Ngara, Kabanga,Rusumo na Rulenge.
Kwa lugha safi, basi angusha comments – umejiandaaje kusherekea Krismasi na kuukaribisha mwaka 2023?
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments