Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Â
Rais mpya wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Bw. John Pombe Magufuli amekiri kuwa wagombea wenzake katika kinyang`anyiro cha kusaka urais, walimpa changamoto kubwa. Akizungumza baada ya kula kiapo katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Bw. Magufuli alisema sasa uchaguzi umekwisha na  yeye ndiye Rais.
“Sasa uchaguzi umemalizika. Rais ni Mimi John Pombe Joseph Magufuli. Tufanye kazi ya kuwatumikia Watanzania ili tusonge mbele,“ alisema Bw. Magufuli mbele ya maelfu ya watu waliohudhuria sherehe hizo.
Aidha aliwaomba kushirikiana naye katika kuwatumikia Watanzania wote bila kujali dini, kabila wala vyama vyao.
Bw. Magufuli aliwashukuru viongozi wa chama chake cha Mapinduzi  (CCM) kwa kumteua kuwania nafasi hiyo iliyokuwa inawaniwa na wafuasi wa chama hicho wapatao 38.
Katika hotuba yake fupi, Bw. Magufuli aliahidi kutimiza ahadi zote alizozitoa wakati wa kamapeni za uchaguzi na akaomba ushirikiano wa viongozi wengine ili kufanikisha malengo yake.
Sherehe za kumuapisha Magufuli na Makamu wake, zilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakiwemo marais wa Kenya, Bw. Uhuru Kenyatta, wa Rwanda, Bw. Paul Kagame wa , wa Uganda Bw. Yoweri Museveni, wa Afrika ya Kusini, Bw. Jacob Zuma na Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe.
Katika hatua nyingine, Rais mtaafu wa awamu ya nne, Bw. Jakaya Kikwete alipata fursa  ya kuwaaga Watanzania baada ya kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka kumi.Hata hivyo alifanya hivyo kwa kuwapungia mikono akiwa kwenye gari la wazi.
Bw. Magufuli tayari ametekeleza jukumu lake la kwanza kwa kumtea Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Mambo yarivyoenda kwenye uapichosho ni kama ifatavyo.
Recent Comments