Recent Comments

Mahafali Yamekamilika, Moonshine Training Institute Huko Kasulo K9

By Baraka Bitariho Dec 18, 2023
Ilikua sio safari rahisi ila hitimisho la hii safari kubwa limekamilika. Hongera sana kwa wanafunzi wote na uongozi mzima wa Moonshine Training Institute iliyop Kasulo K9 Lukole.

Yawezekana kwa wengine, hii ni hitimisho la kwanza katika safari ya kusaka elimu ya juu, pengine kwa wengine wametia nukta katika elimu na kuungana na soko la kazi. Pengine hizi mbio zimefikisha wengine ambapo sasa watategemea wapandishwe vyeo huko wanapobadilisha muda wao kwa mshahara wa kila mwezi.

 

Yakitangazwa mahafali ya tano, tarehe 15 Decementer, 2023, katika chuo cha Moonshine Training Institute kilichopo Ngara Kasulo K9 Lukole Moka wa Kagera.

Kwa hali yoyote, wahitimu wanastahili pongezi kwani safari ya kutafuta usomi sio nyepesi.

 

 

Hawa ni baba, mama, wake, waume, makaka, ama madada ambao wakiwa kwenye harati za kutafuta vyeti vya nyanja mbali mbali, hawakuweka pembeni wajibu wao katika jamiii. Na leo kwa kuwa wamekuwa kioo chema kwa wengi wetu na nguzo bora kwa Ngara, na kwingineko watakapoishia baada ya kuhitimisha masomo yao, their futre is lighten up!

Yakitangazwa mahafali ya tano, tarehe 15 Decementer, 2023, katika chuo cha Moonshine Training Institute kilichopo Ngara Kasulo K9 Lukole Moka wa Kagera.

Pongezi nyingi ziwafikie uongozi na wafanyakazi wote waliopo pale Moonshine Training Institute kwa kuwawekea mazingira bora ya kielimu. Pia hongera kwa hiki chuo kwa kuwa na campus mpya iliyopo Kasulo K9 Lukole na kwa kuona shughuli ya mahafali ya mwaka 2023 inaenda vizuri hususani kwenye campus mpya. Kama picha zinavyoonyesha, kazi haikuwa nyepesi ila imemalizika vizuri.

 

 

Motto ya Moonshine Training Institute ni Let us Light up Your Future.
Na tarehe 15, 12, 2023 Ndayisaba Ruhoro, Mbunge wa Ngara akishuhudia jinsi chuo cha Moonshite kinatimiza ahadi yake kwa jamii, ambayo ni kutoa elimu bora na to light up the future of graduates.
Kwenye meza kuu aliketi pamoja na timu ya wakuu wa chuo hicho kilichopo Ngara Mjini, Kagera.