Majaji wa Marekani wamezuia agizo la Rais Donald Trump lililotaka Mtandao wa TIKTOK wa China uzimwe Nchini Marekani ili kusiwepo na Mtu yeyote anaeweza kuutumia ndani ya Nchi hiyo kuanzia Jumapili ya jana.
Sasa Watumiaji wa Tiktok wataendelea kuitumia kama kawaida Marekani baada ya Majaji kuzuia agizo hilo la Trump saa chache kabla ya Jumapili yenyewe kufika ambapo Trump alisema Mtandao huo wa China ni tishio kwa taifa hilo kwani unaingilia usalama wa Taifa.
Ripoti zinasema maamuzi hayo ya Majaji yameipa TIKTOK ushindi sio wa moja kwa moja bali ushindi kwenye hatua za awali na wataendelea kufanya kazi hadi utakapotolewa uamuzi mwingine.
Iwapo TIKTOK itafutwa Marekani basi kuna Watu 1500 watapoteza ajira kwenye Ofisi za Mtandao huo wa Kijamii ambao ulisema malengo yake pia yalikua ni kuajiri Watu elfu kumi kwenye Ofisi zake za Marekani ifikapo mwaka 2023.
Recent Comments