KAHAMA
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi, ambao majina yao hayajafahamika wameuawa kwa kupigwa mawe na wananchi katika eneo la Manzese Kata ya Busoka Mjini Kahama mkoani wa Shinyanga, baada ya kuvamia duka la fedha maarufu kama M-Pesa,kupora na kutisha watu kwa baruti.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo lietokea Septemba 8mwaka huu, majira ya saa 2:30 usiku, ambapo baada ya majambazi hao kuvamia duka hilo na kufyatua baruti hewani walimshambulia kwa kumpiga mapanga mmiliki wa kibanda cha M-Pesa, Bw. Paulo Charles Inena na kupora pesa za mauzo kiasi cha shilingi Milioni 1, laki 7 na elfu 50
Aidha, katika eneo la tukio kumepatikana silaha moja aina ya shortgun ambayo imekatwa kitako na mtutu, maganda matatu ya risasi za short gun yalitumika kujazia baruti, vocha  mbalimbali za mitandao ya simu na simu moja aina ya Tecno
Recent Comments