Kwa Mara kadhaa,watanzania tumeshuhudia Mh.RAIS wetu kipenzi cha watanzania akitumia Muda wake mwingi,Nguvu zake na Akili zake zote kuwatumikia watanzania usiku na Mchana.Ameonesha Uzalendo kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.
Mh.Rais yupo nyumbani kwake Chato kwa mapumziko mafupi baada ya Ziara na kazi kubwa ya kujenga Taifa.Mapumziko ya Mh.Rais yanatufundisha nini?,Ingalikuwa ni Rais asiye mzalendo wa kweli,Mapumziko haya angeweza kuyafanya nchi za ng’ambo,Marekani,Dubai,Uingereza na Mataifa mengine makibwa yenye Nguvu ya Kiuchumi.
Mh.Rais,kwa kuthamini,Kujali na kutetea maslahi mapana ya kodi za Watanzania,Mh.Rais Yupo Chato kijijini kwake,Amekomaa na Tanzania yake.Najua Jamaa zetu wanatamani sana Mh.Rais asafiri nje ya nchi hata kwa siku moja tu.Lakini Mjomba ni Boda tu Boda.(Home movement).Serikali ya JPM INA sikio la usikivu sana,Kwanini imesikia ?
Vyama vya siasa vilijipatia umaarufu sana kumseama sana Mh.Kikwete na viongozi waliopita kuwa safari zao za nje ya nchi ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Chai Ikulu ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Semina na walsha ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Posho za vikao ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania nk,nk.
JPM,kwa hekima ,unyenyekevu na kwa Sauti ya upole akasema “NIMESIKIA KILIO CHENU” sasa everything STOP.Hakuna safari Nje ya nchi,hakuna posho,hakuna chai ya Ghalama nk,Wakaanza ooooh,Ooooh mbona Rais hasafiri nje jamani!!!!! Oooooh mbona posho hazitoki jamani!!!!!!!,Ooooh Safari za nje wabunge vipi jamani!!!!!!! nk,nk.
“Nimesikia kilio chenu,Sasa ni kila MTU awajibike sawa sawa na Maombi yake” Huyu ndiye Rais anayeendelea kugonga vichwa vya HABARI Duniani nzima kwa utendaji wake,kwa misimamo yake,kwa uzalendo wake,na kwa Uadilifu wake wa hali ya Juu.Lazima tuige mfano wa Kiongozi wetu Mkuu.
Tuendelee kumuombea matashi mema MH.Rais na serikali yake,Tuendelee kuwaombea Viongozi wetu wa chama cha mapinduzi ,Lakini tuendelee kuwaombea pia wale wa upande wa Pili ili waendelee kubatizwa kwa moto.Watanyooka tu.
Mungu Ibariki Tanzania
Recent Comments