Marekani imetoa tahadhari dhidi ya usafiri katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda kufuatia ongezeko la virusi vya corona.
Taarifa katika tovuti ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya imesema serikali ya Kenya imeondoa marufuku ya kukaa nyumbani na kurejesha usafiri na baadhi ya shughuli za kibiashara.
“Zingatia upya uamuzi wa kusafiri Kenya kutokana Covid 19” ilisema tahadhari ya kiwango cha tatu iliyotolewa na CDC ikiangazia usafiri ambao sio wa dhararu.
Tahadhari hiyo inawaarifu wasafiri kwamba mlipuko wa virusi vya corona umeongezeka na kwamba watakua hatarini kupata maambukizo ikiwa hawatakua waangalifu
Mataifa mengine ya Afrika ambayo Sudan Kusini, Ethiopia, Djibouti, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe na nyinginezo.
Huku hayo yakijiri Kenya imemteua mwanariadha bingwa wa Olimpiki mbio za marathon Eliud kuwa balozi wa utalii Kenya wakati taifa hilo likiangalia mianya ya kurejesha utalii wa kimataifa.
Zaidi ya watu milioni mbili wamepoteza ajira zao katika sekta hiyo nchini Kenya na mamlaka inakadiria kuwa hali inaweza kurudi kama awali mwanzoni mwa mwaka 2023.Article share tools
Recent Comments