Mkazi wa mtaa Nhelegani manispaa ya shinyanga Juma Emmanuel(53) anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma ya kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 7 (jina limehifadhiwa)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, ACP Debora Magiligimba,amesema kuwa tukio hilo limetokea Aprili 16 mwaka huu majira ya usiku nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda magiligimba alisema kuwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni kumomonyoka kwa maadili, ambapo Juma alimchukua mtoto huyo usiku kutoka chumba cha kulala watoto na kumpeleka kwenye chumba chake kisha kumuingilia kimwili.
âJeshi la polisi tulipata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo katika eneo la ndembezi kuna mtoto wa kike mwenye umri wawa miaka 7 kubakwa na babu aitwaye Juma ndipo maafisa wa polisi walipofika na kufanikiwa kumtia nguvuni,”alisema Magiligimba.
Taarifa hiyo imesema kuwa mtuhumiwa huyo alipata nafasi ya kufanya kitendo hicho cha kikatili kwa mjukuu wake wakati mke wake wa wa ndoa akiwa amelazwa hospitalini kwa matibabu.
“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika,na kutoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto kwa jeshi la polisi ili kutokomeza vitendo hivyo,”alisema Magiligimba
Recent Comments